Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mpango awafunda Ma-DC, atoa maelekezo saba
Habari za Siasa

Dk. Mpango awafunda Ma-DC, atoa maelekezo saba

Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango
Spread the love

 

MAKAMU wa Rais nchini Tanzania, Dk. Philip Mpango, amewafunda Wakuu wa Wilaya kwa kuwapa maelekezo saba yakuzingatia ili kuwasaidia kutimiza majukumu yao ipasavyo bila kuwa na migongano. Anaripoti Judith Mbasha, DSJ … (endelea).

Amesema Wakuu wa Wilaya ni kiungo muhimu ndani ya serikali katika kutambua na kushughulikia changamoto za wananchi kutokana na kwamba wapo karibu zaidi na wananchi.

Ametoa maelekezo hayo leo Jumatatu tarehe 13 Machi 2023 wakati akifungua mafunzo ya uongizi kwa Wakuu wa Wilaya zote nchini yanayofanyika katika makao makuu ya nchi Dodoma.

Dk. Mapngo amewataka kuhakikisha Wenyeviti wa Vijiji kupitia Mtendaji wanaitisha mikutano ya kijiji na kuwasilisha mpango wa maendeleo pamoja na kutoa mrejesho kwa kusoma taarifa za mapato na matumizi.

Aidha amewataka kujiwekea utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi kwa wakati, “mkawe msaada kwao na sio kero , ninyi ni watumishi wa wananchi na sio mabwana.” Pia amewaagiza kudumisha uhusiano na watumishio walio chini yao kwa kuzingatia kuwa kila mtumishi ana mchango katika kukamilisha utendaji kazi.

“Gharama halisi ya uongozi ni utayari wa kutanguliza mahitaji ya wengine kabla ya mahitaji yako binafsi, au kwa lugha nyingine viongozi mashuhuri ni wale wanaowajali watu ambao wamepewa heshima kuwaongoza, kwahiyo msiende kuwanyanyasa walio chini yenu wanayo mawazo mazuri tu yakuwasaidia katika utendaji wenu wa kazi,” amesema Dk. Mpango.

Makamu wa Rais ameenda mbalizaidi na kuwataka viongozi hao wa wilaya kuepuka migogoro ya kiutendaji na viongozi wenzao “ na hasa Wakurugenzi wa Halmashauri, mhakikishe mnazingatia mipaka yenu ya madaraka na kazi na hatua mtakazochukua daima zizingatie sheria na taratibu za utendaji kazi katika ofisi zenu.”

Sambamba na hilo amewataka kudumisha ushirikiano wa uetendaji kazi na viongozi wenzao ndani ya mihimili yote ya serikali, bunge na mahakama pamoja na viongozi wa chama katika wilaya zao.

Amesema ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi miongoni mwa vigezo vya kupima tija kwenye halmashauri na uwezo wa kukamilisha kazi kwa viwango na muda uliopangwa.

“Napenda niwaambie waziwazi hatutaendelea kuvumilia uzembe, ubadhirifu na kukosa uaminifu na ubunifu. Kasimamieni tija ya utendaji katika maeneo yenu , elimu mtakayopata hapa mkaitumie ili kuondoa dosari za utendaji zinazoweza kujitokeza,” amesema Dk. Mpango.

Metawakata pia kuongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali na kudhibiti uvujai wa mapato, kusimamia maadili na nidhamu kazini na kuhudumia wananchi kwa lugha ya staha.

Pia amewataka kusimamia suala la usafi na uhifadhi wa mazingira wa nchi kwani dunia inakabiliwa na changamoto mbalimali ikiwemo mabailiko ya tabia ya nchi, kutoweka kwa bayoanuwai na uharibifu wa mazingira.

Mwisho amewataka kujijengea tabia ya kujiongezea ujuzi kwa njia mbalimbali ikiwemo matumizi ya mitandao, “kuna maarifa huko nyie ni watu wazima msiende kutafuta mambo ya hovyo, someni vitabu, taarifa mbambali na takwimu juu ya viashiria vya maendeleo na kupata busara kwa viongozi ambao wamepita kwenye nyadhifa mbalimbali ili muwe wabunifu na kuepuka kufanya mambo kwa mazoea.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!