Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wafanyakazi NMB wagawa magodoro, kompyuta magereza ya Chato, Kasungamile
Habari Mchanganyiko

Wafanyakazi NMB wagawa magodoro, kompyuta magereza ya Chato, Kasungamile

Spread the love

KATIKA kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita kwenye kuhudumia wananchi, Wafanyakazi wa benki ya NMB kutoka matawi ya Chato na Sengerema wametoa msaada wa magodoro 50 katika gereza la wilaya ya Chato pamoja na kompyuta moja na UPS kwa gereza la Kasungamile wilayani Sengerema. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo yaliyofanyika katika gereza la Kasungumile wilayani Sengerema, Meneja wa benki ya NMB – Stanley Betty alisema benki ya NMB tawi la Sengerema ilipokea ombi la hitaji ya kompyuta kutoka uongozi wa gereza la Kasungamile na benki yao ikaona ifanikishe ombi hilo.

“Benki yetu ya NMB itaendelea na juhudi mbali mbali za kuunga mkono Serikali ya awamu ya sita katika kuleta maendeleo” alisema Betty.

Amepongeza watumishi wa gereza la Kasungamile kwa kuendelea kutumia huduma za benki ya NMB. 

Naye Kaimu Mkuu wa Gereza la Kasungamile – Hiyari Mwaijombe alishukuru benki ya NMB kwa msaada wao.

“Kompyuta tuliyopewa itaturahishia katika kazi zetu za kila siku ikiwemo kuwaandalia wafungwa rufaa pamoja na mahitaji yao mengine mbali mbali” alisema Mwaijombe. 

Aliongezea kuwa  inawaomba benki ya NMB iweze kuwasaidia uhitaji wa matenki mawili yenye ujazo wa lita 5000 kwajili ya kutunzia maji katika gereza lao na upatikanaji wa taulo za kike kwa wafungwa sita wanawake waliopo katika gereza la Kasungamile. 

Naye, Meneja wa benki ya NMB Wilaya ya Chato – Baraka Nyagwaswa ameshukuru uongozi wa gereza la Chato kwa kupokea msaada wa magodoro 50 kutoka benki ya NMB.

“Kwa hapa Chato sisi ni wenyeji sana na tunajiona wenyeji zaidi kwa kutambua kuwa tunatambulika na kushirikishwa katika masuala muhimu kwa maendeleo,ushirikiano huu ndio unatafanya kuwa benki yenye kujali umuhimu wa masuala ya jamii” alisema Nyagwaswa.

Aliahidi kuwa benki ya NMB itaendelea kuunga mkono juhudi za wadau wake wakubwa katika kuhakikisha kuwa changamoto za jamii zinapatiwa ufumbuzi katika kujenga afya na elimu bora kwa jamii ya Tanzania.

Aidha, Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Chato, Raphael Magesa ameishukuru benki ya NMB na kuwaomba pia Wadau wengine iwasaidie magodoro mengine zaidi, vyakula na sabuni kwani wafungwa na mahabusu wanauhitaji huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!