Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Samia amlilia Papa Benedikto XVI
Habari Mchanganyiko

Dk. Samia amlilia Papa Benedikto XVI

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan ameeleza kusikitishwa na kifo cha Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI aliyefariki dunia leoJumamosi saa 3: 34 Asubuhi tarehe 31 Desemba 2022 akiwa na umri wa miaka 95.

Rais Samia amesema Baba Benedikto alijitoa maisha yake kutumia wengine. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika ujumbe wake alioutoa kupitia mtandao wa Twitter Dk. Samia ametuma salama za pole kwa Baba Mtakatifu Francisko na waumini wa Kanisa Katoliki na duniani kote.

“Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Baba Mtakatifu Mstaafu Benedict XVI, ambaye alijitoa maisha yake kutumikia wengine. Natuma salamu za pole kwa Baba Mtakatifu Francisko, waumini wa Kanisa Katoliki Tanzania na Duniani kote. Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi. Amina”.

Baba Benedikto amefikwa na umauti akiwa katika makazi yake kwenye Hosteli ya Mater Ecclesiae iliyoko kwenye Bustani za Vatican ambako alikuwa anaishi tangu mwaka 2013 alipong’atuka kutoka madarakani kutokana na sababu za umri kuwa mkubwa.

Alifanya maamuzi haya magumu, ili kutoa nafasi kwa kiongozi mwingine, aweze kulitumikia Kanisa la Kristo Yesu, kwa ari na moyo mkuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!