MAZISHI ya Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI aliyefariki dunia leoJumamosi saa 3: 34 Asubuhi tarehe 31 Desemba 2022 akiwa na umri wa miaka 95, yatafanyika Alhamis tarehe 5 Januari na yataongozwa na Papa Francis. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea).
Baba Benedikto amefikwa na umauti akiwa katika makazi yake kwenye Hosteli ya Mater Ecclesiae iliyoko kwenye Bustani za Vatican ambako alikuwa anaishi tangu mwaka 2013 alipong’atuka kutoka madarakani kutokana na sababu za umri kuwa mkubwa.
Alifanya maamuzi haya magumu, ili kutoa nafasi kwa kiongozi mwingine, aweze kulitumikia Kanisa la Kristo Yesu, kwa ari na moyo mkuu.
Kwa mujibu wa Vatican News wamealikwa watu mbalimbali kuungana na Mama Kanisa kwa ajili ya kumwombea maisha ya uzima wa milele Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI.
Aidha, Kiongozi wa Ujerumani ametoa salamu za rambirambi kwa mjerumani mwenzake.
Kansela Olaf Scholz ametuma ujumbe wake kwenye mtandao wa Twitter akisema Papa huyo wa zamani alikuwa “kwa wengi, sio tu katika nchi hii, kiongozi maalum wa kanisa”, amesema.
Leave a comment