Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ateta na Mbowe, Kinana Ikulu Dar
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ateta na Mbowe, Kinana Ikulu Dar

Spread the love

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokea taarifa ya Maendeleo ya mazungumzo ya mchakato wa maridhiano ya kisiasa, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Desemba 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu- Rais Samia amepokea taarifa hiyo kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana

Hii ni mara ya pili kwa Rais Samia kukutana na Mbowe kwa ajili ya mazungumzo hayo kwani mara ya kwanza, alikutana na Mbowe tarehe 4 Machi, 2022, Ikulu ya Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalijiri saa chache baada ya Mbowe kuachiwa huru kutoka gerezani alikokaa kwa zaidi miezi tisa kwa tuhuma za ugaidi.

Pamoja na mambo mengine kikao chao hicho kilitajwa kufungua milango ya vikao vingine vya maridhiano ya kisiasa baina ya viongozi wa vyama hivyo.

Itakumbukwa kuwa Tume ya watu 10 kutoka Chadema iliundwa sambalba na idadi kama hiyo kutoka CCM na kukutana Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma kuanza mazungumzo hayo.

Licha ya Mbowe kupata upinzani kutoka kwa baadhi ya viongozi na wafuasi kutoka Chadema, mara kwa mara alisisitiza kuendelea na mazungumzo hayo kwani ndio njia sahihi ya kufikia muafaka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bunge labaini madudu mfumo ukusanyaji mapato, h’shauri tatu kikaangoni

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba...

Habari za Siasa

Mbunge afurahia mabilioni ya Samia kutua jimboni

Spread the love  MBUNGE wa Igunga, Nicholas Ngassa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji...

Habari za Siasa

PIC yaishauri Serikali kuanzisha mfuko wa uwekezaji kusaidia mashirika ya umma

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji...

error: Content is protected !!