Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ripoti ya ajali ya ndege Bukoba: Vikosi vya uokoaji vilichelewa kufika
Habari MchanganyikoTangulizi

Ripoti ya ajali ya ndege Bukoba: Vikosi vya uokoaji vilichelewa kufika

Ndege ya Precision ikiwa imezama katika ziwa Victoria baada ya kushindwa kutua uwanja wa Ndege wa Bukoba, Kagera
Spread the love

TAARIFA ya awali ya ripoti ya ajali ya ndege ya shirika la Precision iliyotokea katika eneo la Ziwa Victoria Tanzania, imetolewa leo Jumanne na wizara ya ujenzi na uchukuzi nchini na kuonesha kuwa vikosi vya uokoaji vilichelewa kufika katika eneo la tukio. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma …  (endelea).

Ajali hiyo ilitokea muda wa saa 2 asubuhi saa tarehe 6 Novemba, 2022, lakini kwa mujibu wa ripoti hiyo inaeleza kuwa boti ya kitengo cha polisi wa majini, ilifika muda wa saa saba saa za Tanzania.

‘’ Boti ilifika saa saba eneo la tukio, baada ya kufika walikua na changamoto ya kuishiwa mafuta na oksijeni, kabla hawajafika, mvuvi mmoja tayari alianza kutoa maiti zilizokuwa ndani ya ndege’’ taarifa ya ripoti inasema.

Taarifa ya ripoti hiyo pia haijatoa sababu kamili ya nini kilisababisha kutokea kwa ajali, ikisema kuwa uchunguzi bado unaendelea.

Mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania awali ilibainisha kuwa baada ya ripoti ya awali itafuatia ripoti ya uchunguzi wa awali inayotarajiwa kuchapishwa mwezi mmoja baada ya ajali na kisha ripoti kamili baada ya mwaka mmoja.

Ndege hiyo ya shirika la precision ATR 42-500 yenye namba PW 494 ilianguka kwenye ziwa Victoria mita chache kutoka uwanja wa ndege wa Bukoba, ikijiandaa kutua ikitokea jijini Dar es Salaam kupitia Mwanza.

Ajali hiyo iliua watu 19 kati ya 43 waliokuwemo akiwemo rubani na msaidizi wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!