Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yatoa msaada sekta ya afya Tanga, yapongezwa
Habari Mchanganyiko

NMB yatoa msaada sekta ya afya Tanga, yapongezwa

Spread the love

VIONGOZI wa wilaya ya Mkinga Mkoa wa Tanga wamepongeza maono na fikra za uongozi wa Benki ya NMB nchini, kwa kusaidia sekta ya afya hasa huduma ya mama na mtoto wilayani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Pongezi hizo zimetolewa jana Jumatano tarehe 9 Novemba 2022 wakati wa kukabidhi vitanda viwili na mashuka 100 kwa ajili ya kituo cha afya Mkinga vikiwa na thamani ya zaidi ya sh milioni tatu.

Mkuu wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Sulumbu (watatu Kulia) akipokea kitanda cha kujifungulia kutoka kwa Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini, Dismas Prosper (watatu Kushoto) katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa kituo cha afya cha Mkinga. Hafla hii ilishuhudiwa na Mganga mkuu wa wilaya ya Mkinga, Dk. Joseph Ligoha (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya Mkinga, Zahra Msangi (kulia)

Akizungumza katika hafla hiyo Mganga Mkuu wa wilaya ya Mkinga, Dk. Joseph Ligoha alisema msaada huo umetolewa kwa wakati muafaka kwa kuwa mahitaji ya vifaa tiba katika zahanati na vituo vya afya, katika wilaya hiyo ni mkubwa.

Dk Ligoha alisema maono ya NMB ya kutoa vifaa vya afya vya huduma ya mama na mtoto, ni mawazo sahihi kwasababu mara nyingi idadi ya akina mama wanaojifungua imekuwa ikiongezeka na kuwa na vitanda vichache.

“Tunawashukuru NMB aliyebuni na kutoa msaada huu, tunampongeza sana, ni msaada utakaowasaidia huduma ya mama na mtoto lakini si hivyo tu hata kuokoa maisha ya watanzania walio wengi, ” alisema Dkt Ligoha.

Alisema hata ukichukua changamoto ya maji iliyokuwepo katika kituo hicho cha afya, mashuka yatasaidia kupunguza tatizo la wagonjwa kulazwa wakiwa na mashuka ya nyumbani ambayo yanaweza kuzusha magonjwa mengine.

“Tatizo la maji ni kubwa juhudi tunazozifanya kuzuia matumizi ya nguo za nyumbani ili zisilete magonjwa mengine na mashuka haya mliotupa yataisaidia katika zahanati yetu,” alisema Dk. Ligoha.

Dk. Ligoha alisema NMB si mara moja ama mbili wamekuwa wadau wakubwa katika wilaya hiyo ambapo mwaka jana waliisaidia zahanati ya   Mwandusi vifaa vya mama na mtoto ikiwemo Oxygen.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Zahra Msangi aliishukuru NMB kwa msaada huo ambao alisema umekuja kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha suala la uzazi salama linawekewa mpango mkakati.

Alisema NMB wamekuwa ni sehemu ya familia ya wilaya hiyo kwakuwa wamekuwa wakiwasaidia na wamewaomba waendelee kuwashika mkono hasa ukizingatia mapato yao ya ndani hayatoshelezi mahitaji ya kijamii.

Mkuu wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Sulumbu, aliishukuru NMB kwa msaada huo kwa kueleza kwamba sera ya serikali sasa ni kuboresha huduma za afya baada ya kujengwa Vituo vya afya kila kata.

“Sera ya nchi ni kujenga vituo vya afya kila kata, Rais alisema sasa tutazame huduma tunazotoa kwa wananchi badala ya kujenga vituo vingi…Wenzetu wa NMB kabla Rais hasema nyie mmekwenda mbele zaidi kusaida vifaa tiba, hongereni sana,” alisema Mkuu huyo wa wilaya na kuongeza kwamba serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa benki hiyo ili waweze kutimiza na kutoa huduma kwa wananchi.

Awali, Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa benki hiyo ya NMB Dismas Prosper alisema benki hiyo inaishukuru na kuipongeza uongozi wa wilaya ya Mkinga kwa kuwa karibu na benki hiyo na kushirikiana nao katika mambo mbalimbali ya Maendeleo ya jamii.

“Kwa hapa Mkinga sisi ni wenyeji zaidi tunatambulika na tunashirikishea katika Maendeleo ya jamii ambapo ushirikiano huo ndiyo unaoifanya benki hiyo kuwa kinara katika kujali na kujihusisha na masuala ya kijamii nchini.

Alisema kwa mwaka huu imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 2 kutoka katika asilimia moja ya mapato yake ya kila mwaka, kuzirudisha kusaidia huduma za afya na elimu kwa jamii.

Alisema benki hiyo inatambua jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini na ndiyo maana wameamua kuiunga mkono.

“Changamoto ya sekta ya afya nchini Tanzania kwa benki ya NMB ni suala la kipaumbele…Hii ni kutokana na ukweli kwamba afya ni muhimu kwa Maendeleo hapa nchini,” alisema na kuongeza

“NMB inatambua juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kusimamia upatikanaji wa afya bora kwa kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma hizo, pamoja na juhudi hizo za serikali sisi kama wadau tubawajibu wa kuunga mkono juhudi hizo,” alisema.

Hafla hiyo iliyofanyika katika katika kituo cha afya hicho, mbali na kuhudhuriwa na watumishi, wananchi wa maeneo ya jirani pia walikuwepo madiwani wakiongozwa na Makamo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Kadiri Mwaliza na diwani wa kata ya Parungu Kasera Mwajasi Bamilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

Habari Mchanganyiko

GGML yaja na teknolojia za kisasa maonesho ya OSHA Arusha

Spread the loveKATIKA kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na...

error: Content is protected !!