Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mkurugenzi Dewa Logistics na wenzake kizimbani kuitia hasara TRA 487 mil
Habari Mchanganyiko

Mkurugenzi Dewa Logistics na wenzake kizimbani kuitia hasara TRA 487 mil

Spread the love

 

MKURUGENZI wa Dewa Trading Logistic Ltd, Erasto Dewa na wenzake wawili wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka manne ikiwemo la kukwepa kodi na kuisababishia mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hasara ya zaidi ya Sh.487 milioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mashtaka mengine ni Kuchepusha bidhaa kutoka njia yake iliyotengwa na kuwasilisha nyaraka za uongo.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Mwandamizi kutoka TRA, Medalakini Emmanuel akisaidiana wakili Neema Moshi imewataja washtakiwa wengine kuwa ni, Ramadhani Salum na Frank Mgata.

Mbele ya Hakimu Francis Mhina imedaiwa washtakiwa wametenda makosa hayo kati ya tarehe 21 Septemba na 28, 2022 huko Tabata, ndani ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Katika shtaka la kuchepusha bidhaa kutoka kwenye njia yake iljyotengwa inadaiwa, Septemba 28, 2022 huko katika eneo la Tabata, washtakiwa kwa pamoja walifanya ulaghai kwa kuchepusha bidhaa za vitenge kutoka njia iliyotengwa ya kutoka Dar es Salaam kwenda Malawi na kupakua bidhaa hizo katika eneo la Tabata jijini Dar es Salaam.

Katika shtaka la tatu linalomkabili mshtakiwa Dewa peke yake inadaiwa, Septemba 21, 2022 kwa udanganyifu alitoa tamko la uongo la maelezo ya shehena ya marobota 290 kama mashuka badala ya vitenge.

Katika shtaka la mwisho inadaiwa Septemba 28, huko Tabata, washtakiwa wote kwa pamoja kutokana na matendo yao ya ukwepaji kodi, waliisababishia TRA hasara ya Sh. 487,945,210.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi Novemba 24, 2022.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

error: Content is protected !!