Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Pareso aiambia mahakama alihofia usalama wake wito Chadema
Habari za Siasa

Pareso aiambia mahakama alihofia usalama wake wito Chadema

Spread the love

 

MBUNGE Viti Maalum, Cecilia Pareso, amedai alishindwa kufika katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema, cha tarehe 27 Novemba 2020, kujibu tuhuma zilizokuwa zinamkabili za kujiteua na kujipeleka bungenj jijini Dodoma, kutokana na kuhofia usalama wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pareso ametoa madai hayo leo Jumanne tarehe 8 Novemba, 2022, akiulizwa maswali ya ufafanuzi na wakili wake, Edson Kilatu, kwenye Mahakama Kuu, Masijala Kuu, jijini Dar es Salaam, mbele ya Jaji Cyprian Mkeha.

Wakili Kilatu alimhoji kwa nini alishindwa kufika mbele ya kikao hicho, ambapo alidai ni kutokana na taharuki iliyoibuka kufuatia hotuba iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, ya tarehe 24 Novemba 2020, baada ya kuapishwa kuwa mbunge wa viti maalum, tarehe 23 Novemba mwaka huo.

“Nilizungumzia kuhusu usalama wangu na katika barua yangu niliyoandika kuomba ahirisho la wiki moja nilisema kutokana na usalama wangu, kuwepo kwa vitisho vya maandamano kutoka kwa wafuasi wa Chadema.

Wakili wa Chadema, wakiongozwa na Peter Kibatala (katikati) wakiwa mahakamani

Wakili Kilatu alikuwa anamuuliza maswali ya ufafanuzi dhidi ya maswali ya dodoso aliyoulizwa na Wakili wa Chadema, Peter Kibatala, kuhusu madai yake ya kuvuliwa uanachama kinyume cha Sheria, bila kupewa haki ya kusikilizwa.

Ni katika kesi Na. 36/2022, iliyofunguliwa na wabunge viti maalum 19, wakiongozwa ba Halima Mdee, dhidi ya Chadema, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), wakiiomba mahakama ifanye mapitio ya mchakato uliotumiwa na Chadema kuwavua uanachama, wakidai haukuwa halali kwa kuwa walinyimwa haki ya kusikilizwa.

Baada ya Wakili Kilatu kumaliza kumhoji maswali ya ufafanuzi, Jaji Mkeha aliahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumatano, ambapo Mbunge Viti Maalum, Jesca Kishoa, ataanza kuulizwa maswali ya dodoso na mawakili wa Chadema, kuhusu madai aliyowasilisha mahakamani hapo kupitia hati yake ya kiapo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

error: Content is protected !!