Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Michezo Majaliwa mgeni rasmi mbio za NMB Marathon 2022
Michezo

Majaliwa mgeni rasmi mbio za NMB Marathon 2022

Spread the love

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya mbio za NMB Marathon 2022 yanayotarajiwa kufanyika Oktoba mosi katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mashindano hayo yanayoratibiwa na Benki ya NMB yamesogezwa mbele ili kukidhi maombi ya washiriki wengi ambapo hapo awali yalipangwa kufanyika Septemba 24 mwaka huu.

Meneja Rasilimali Watu wa benki hiyo, Emmanuel Akonaay (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya NMB Marathon, Mercy Nyange (kushoto) kwa pamoja wakionesha vifaa vitakavyotumika katika mbio za NMB Marathon 2022 zinazotarajiwa kutimua vumbi Oktoba mosi mwaka huu katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana katika uzinduzi wa ‘kits’ vifaa vya mbio hizo, Meneja Rasilimali Watu wa benki hiyo, Emmanuel Akonaay alisema mashindano hayo yanalenga kuchangia matibabu ya fistula kwa wanawake kupitia Hospitali ya CCBRT.

Alisema katika mbio hizo ambazo zitashirikisha wadau wa aina mbalimbali, jumla ya Sh milioni 600 zimepangwa kukusanywa ili kusaidia matibabu ya akina mama wenye matatizo hayo ya fistula.

“Kwa siku 10 hizi zilizobaki tunaomba Watanzania na wadau mbalimbali na kampuni, kujisajili kushiriki mbio hizi ili kuchangia matibabu hayo,” alisema na kuongeza kuwa kauli mbio ya mbio hizo ni ‘mwendo wa upendo’.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya NMB Marathon, Mercy Nyange alisema hadi kufikia jana Septemba 20, 2022 jumla ya washiriki 3000 wamejisajili katika mbio hizo.

“Tunawaomba Watanzania na wadau mbalimbali kusogea pale Juliana Pub Mbezi Beach, Mtana Bar au Mlimani City kwa siku hizi 10 zikizobaki ili wajisajili na kuwa kwenye orodha rasmi ya wale watakaokimbia kwenye NMB Marathon 2022,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Uingereza, Hispania, Italia na Ufaransa kinawaka leo

Spread the loveLIGI mbalimbali barani ulaya kuendelea leo na michezokadhaa mikali itakwenda...

Michezo

Leo mkwanja upo Meridianbet, usipishane nao

Spread the love  Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Michezo

Anza wikendi yako na Meridianbet, upige mkwanja wa maana

Spread the love Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Habari MchanganyikoMichezo

Arafat atoka bima na kurejea kwenye benki

Spread the loveRais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amemteua Arafat Ally Haji kuwa...

error: Content is protected !!