Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari Yanga yaanza safari ya kutetea ubingwa wake
HabariMichezo

Yanga yaanza safari ya kutetea ubingwa wake

Spread the love

 

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Polisi Tanzania. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Yanga imeanza kampeni yake kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Wenyeji wa mchezo huo Polisi Tanzania ilikuwa ya kwanza kupata bao hilo, kupitia kwa Salum Ally Kipemba dakika ya 34 Kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo.

Polisi wanaandikisha bao hilo, muda mchache mara baada ya mshambuliaji wa klabu ya Yanga Fiston Mayele kukosa mkwaju wa penati kwenye dakika ya 10 mara baada ya winga wa klabu hiyo Jesus Moloko kuangushwa kwenye eneo la hatari.

Mara baada ya kukosa mkwaju huo wa penati, kwenye dakika ya 41, Mayele alirudi tena kambani kwa kuandika bao la kusawazisha na kufanya mchezo huo Kwenda mapumziko wakiwa sare ya bao 1-1.

Kwenye kipindi cha pili cha mchezo kocha wa klabu ya Yanga, Mohammed Nasreddine Nabi alifanya mabadilo ya wachezaji wa wawili kwa kumuingiza Uwanjani Feisal Salum aliyechukua nafasi ya Gael Bigirimana sambamba na Bernad Morrison aliyechukua nafasi ya Dikson Ambundo.

Mabadiliko hayo yalileta matokeo chanya kwa mabingwa hao watetezi ambapo mara baada ya kulisakama lango la Polisi Tanzania kwa muda mrefu kwenye dakika ya 84, Nahodha wa klabu hiyo Bakari Nondo Mwamnyeto alifanikiwa kuandika bao la pili na la ushindi kwenye mchezo huo.

Kwa matokeo hayo, Yanga imeenda kileleni kwa mara ya kwanza mara baada ya kupigwa kwa michezo minne mpaka sasa.

Mabingwa hao watetezi wataendelea kusalia jijini Arusha ambapo, Jumamosi tarehe 20 Agosti 2022, watashuka tena kwenye dimba hilo dhidi ya Coastal Union ambao watalazimika kutumia uwanja huo, mara baada ya dimba la CCM Mkwakwani kufungiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

Michezo

Beti na Meridianbet mechi za leo

Spread the love IKIWA leo hii ni Jumapili tulivu kabisa, Meridianbet wanamkwambia...

error: Content is protected !!