Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Magari kupita daraja jipya la Wami Septemba mwaka huu
Habari Mchanganyiko

Magari kupita daraja jipya la Wami Septemba mwaka huu

Spread the love

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa Serikali inatarajia kuanza kuruhusu magari kupita juu ya daraja jipya la wami, lililopo mkoani Pwani ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.

Hayo yamesemwa leo tarehe 16 Agosti, 2022 na Waziri huyo wakati akikagua hatua za maendeleo ya daraja hilo ambapo pamoja na mambo mengine amemtaka mkandarasi kukamilisha kazi ndogo ndogo zilizobakia katika daraja hilo ili kurahisisha matumizi salama ya watumiaji wa daraja hilo.

“Hadi sasa kazi zinaendelea vizuri, ni matumaini yangu hadi kufikia tarehe 20 Septemba, mtakuwa mmeshakamilisha kazi zilizobaki ili mimi niweze kuruhusu magari kupita”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Ameeleza kuwa mradi huo ambao umefikia asilimia 86 katika utekelezaji wake unajumuisha  ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 513.5  pamoja na ujenzi wa barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 3.8.

Aidha, amemshukuru Rai Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya kimkakati na kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji nchini.

Akitoa taarifa ya mradi, Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Pwani Mhandisi Heririsper Mollel, ameeleza kuwa kwa upande wa ujenzi wa  daraja mkandarasi amekamilisha ujenzi wa sehemu ya chini ya daraja kwa asilimia 100 na sehemu ya juu amekamilisha tabaka la juu la lami mita 256 kati ya mita 513.5 ambayo ni sawa na asilimia 50 ya urefu wa daraja.

Ameongeza kuwa kazi nyingine zilizokamilika ni ujenzi wa makalvati makubwa matatu na madogo saba na uwekaji wa mabomba 188 ya maji kati ya 206 ambayo ni sawa na asilimia 91.

Kuhusu ujenzi wa barabara unganishi  Mhandisi Heririsper amesema kuwa hadi sasa kilometa 3.4 za ujenzi wa tabaka la lami la chini zimekamilika.

Ujenzi wa Daraja jipya la Wami unagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 75 ambazo ni fedha za Serikali  kwa asilimia 100 na unatekelezwa na mkandarasi Power Construction  Corporation kwa muda wa miezi 48.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!