Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Odinga aibuka, ahubiri amani, maridhiano
KimataifaTangulizi

Odinga aibuka, ahubiri amani, maridhiano

Spread the love

MGOMBEA urais nchini Kenya kupitia muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga jana Agosti 14, 2022 ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu siku ya uchaguzi tarehe 9 Agosti na kutoa ujumbe wa kudumisha amani kwa raia wa taifa hilo la Afrika Mashariki. Anaripoti Mwandishi … (endelea).

Jana Jumapili Odinga amehudhuria ibada katika kanisa la Mtakatifu Francis ACK lililopo huko Karen jijini Nairobi huku akiwa ameambatana na Mgombea mwenza, Martha Karua.

Pia Odinga aliambatana na viongozi wa chama chake ODM pamoja na washirika wake akiwamo Mwenyekiti wa Kanu, Gideon Moi na Mbunge mteule wa Lang’ata, Phelix Kodhe.

Akiwa kanisani Raila alinukuu Sala ya Mtakatifu Francis Asizi inayosema,”Bwana, utufanyie vyombo vya amani yako. Palipo na chuki na tupande upendo; penye madhara, msamaha; penye ugomvi, umoja….”

Pamoja na sala hiyo Odinga alisema anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumvusha salama katia kipindi cha kampeni n ahata zoezi la upigaji kura.

“Huko kote kulikuwa na changamoto lakini tumevuka kwa amani ni matumaini yangu kwamba amani itaendelea kutawala taifa letu hata baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa kwa sababu sisi ni sehemu ya taifa hili na Kenya itaendelea kuwa imara hata baada ya uchaguzi,” amesema.

Alisema yeye ni Mkenya hivyo anatamani kuona amani, umoja na upendo vikiendelea kutawala taifa hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!