Sunday , 12 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wapiga kura wampokea kishuja Odinga, wasukuma gari
Kimataifa

Wapiga kura wampokea kishuja Odinga, wasukuma gari

Spread the love

 

MGOMBEA urais wa muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga mapema leo saa 4:00 asubuhi amewasili katika Shule ya msingi ya Old Kibra ambayo ndio kituo chake cha kupiga kura na kupokewa kishujaa na maelfu ya wapiga kura nchini Kenya. Anaripoti Mwandshi Wetu, Kenya … (endelea).

Raila ambaye ni mmoja kati ya wagombea wanne wa uchaguzi wa urais mwaka 2022, amekuwa wa mwisho kupiga kura yake baada ya awali wagombea wengine kama William Ruto wa UDA akiwa wa kwanza kupiga kura yake eneo la Sugoi.

David Mwaure wa Agano alipiga kura yake pia maeneo ya Upperhill Nairobi akifuatiwa na wakili msomi George Wajackoyah ambaye alifika maeneo ya Matungu dakika chache mbele ya Odinga.

Hata hivyo, Wajackoyah alishindwa kupiga kura kwa wakati baada ya mtambo wa KIEMS kushindwa kumtambua na kumfanya asubiri kwa muda zaidi ili kuona kama atapiga kura.

Raila aliwasili katika kituo hicho huku akilakiwa na mamia ya wafuasi wake waliomsubiri kwa mbwembwe kumkaribisha Old Kibra na baada ya kupiga kura walimsindikiza kwa kulisukuma gari lake hadi nje ya kituo hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

error: Content is protected !!