Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wachimbaji wadogo Ulanga wapigwa msasa matumizi ya baruti
Habari Mchanganyiko

Wachimbaji wadogo Ulanga wapigwa msasa matumizi ya baruti

Spread the love

 

OFISI ya Tume ya Madini Mahenge imeendesha mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini wanaoendesha shughuli zao katika Wilaya ya Ulanga ili kuwajengea uwezo wa namna bora ya matumizi ya baruti kwenye shughuli za madini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Akizungumza kwenye mafunzo hayo ya siku tano, Mhandisi Migodi wa Ofisi ya Madini Mahenge, Joseph Ng’itu amewataka wachimbaji wadogo kuendelea kujifunza zaidi teknolojia ya ulipuaji na baruti ambayo imekuwa ikibadilika mara kwa mara.

Aidha, amewataka wachimbaji wadogo kuhakikisha wanaendesha shughuli zao kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanapata cheti cha kulipulia na kusisitiza kuwa ofisi ya madini ipo tayari kutoa kwa watakaoomba.

Akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo hayo mapema jana tarehe 15 Julai, 2022 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ulanga, Abraham Mwaikwila amewataka washiriki wote kuzingatia yale waliyofundishwa hususan usalama wa matumizi ya baruti.

Pia amewatka kutekeleza Sheria na Kanuni za Baruti ipasavyo na kuachana na tabia ya kufanya shughuli za milipuko kimazoea pasipo kuzingatia utaalamu.

Pia amewataka wachimbaji wadogo hao kuwa mabalozi wazuri kwa wachimbaji wengine wadogo kwa kuwaelimisha Sheria na Kanuni zinazosimamia baruti ili nao waweze kutekeleza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!