Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wananchi wavamia ‘swimming pool’ Ikulu, Rais akimbia
Kimataifa

Wananchi wavamia ‘swimming pool’ Ikulu, Rais akimbia

Spread the love

 

RAIS Sri Lanka, Gotabaya Rajapaksa leo tarehe 9 Julai, 2022 ameripotiwa kuhamishwa na kupelekwa mahali salama baada ya makundi ya watu kuvunja kizuizi kilichokuwa kimewekwa na maofisa wa polisi na kuingia ikulu ya nchi hiyo. Amaripoti Mwandishi Wetu … (emdelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya kuibuka kwa maandamano makubwa ambayo yamesababishwa na mdororo wa uchumi tangu nchi hiyo ya Kusini mwa Bara la Asia ipate uhuru huku ikikumbwa na uhaba mkubwa wa mafuta na madawa.

Makumi kwa maelfu ya waandamanaji wanaomtaka Rais Rajapaksa na serikali yake wajiuzulu wamevamia makaazi yake rasmi leo Jumamosi na kuingia Ikulu kisha kuanza kupiga picha na kuogelea kwenye swimming pool lililopo katika jumba hilo.

Rajapaksa amepelekwa mahali salama, amesema Ofisa mmoja katika ofisi yake alipokuwa akizungumza na shirika la habari la DPA.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!