Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Waziri Mkuu Sri Lanka akubali kujizulu
Kimataifa

Waziri Mkuu Sri Lanka akubali kujizulu

Spread the love

 

Waziri Mkuu wa Sri Lanka, Ranil Wickremesinghe amekubali kujiuzulu baada ya viongozi wa vyama vya siasa nchini humo kumtaka yeye na rais aliye madarakani kukaa kando. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). 

Hatua hiyo imetokana na shinikizo la waandamanaji ambao wameyavamia makazi yake na kuyachoma moto kutokana na kughadhibishwa na mdororo wa kiuchumi.

Msemaji wa waziri mkuu, Dinouk Colambage, amesema Wickremesinghe amewaambia viongozi wa chama kwamba atajiuzulu pale ambapo pande zote zitakapokubaliana katika namna ya uundwaji wa serikali mpya.

Ametoa uamuzi huo leo tarehe 9 Julai, 2022 baada ya kufanyika kwa maandamano makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Sri Lanka.

Maelfu ya watu walivunja vizuizi na kuingia kwenye makazi ya Rais Gotabaya Rajapaksa na ofisi iliyo karibu kwa kuonesha hasira zao kwa kiongozi huyo.

Picha za video ziliwaonesha mamia ya waandamanaji wakiwa katika bustani yenye bwawa katika makazi hayo na wengine wakiwa na nyuso za furaha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!