Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Viongozi CHASO wataja sababu za kuikacha kuhamia ACT-Wazalendo
Habari za Siasa

Viongozi CHASO wataja sababu za kuikacha kuhamia ACT-Wazalendo

Spread the love

 

BAADHI ya waliokuwa viongozi na wanachama wa Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati wa Chadema (CHASO), wametaja sababu nne za kuhamia Chama cha ACT-Wazalendo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Sababu hizo zimetajwa leo Jumamosi, tarehe 25 Juni 2022 na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti na Mratibu wa CHASO, Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Abdul-Aziz Ally Carter, siku chache baada ya kuhamia ACT-Wazalendo na kupokelewa na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Ado Shaibu.

Carter ametaja sababu ya kwanza ni kuwa ni mgongano wa kifikra, akidai ndani ya CHASO kuna changamoto hiyo.

“Ndani ya CHASO kumekuwepo na mgongano wa kifikra. Wakati wenzetu waliobaki walitaka kuwa CHASO ijikite zaidi na harakati za ndani ya Chuo hasa kupigania maslahi ya Wanafunzi, baadhi yetu tuliona kufanya hivyo ni kupuuza mchango wa Vyuo Vikuu katika ukombozi wa jamii,”

“Tunaondoka CHASO ili tuiache iendelee na maono yao ya kujikita kwenye harakati finyu (narrow) za Chuoni nasi tutimize ndoto zetu za harakati pana ya kuikomboa jamii,” amedai Carter.

Sababu nyingine zilizotajwa na Carter ni “kwa muda mrefu tumekuwa haturidhishwi na jinsi CHASO imekuwa ikishiriki kusaidia harakati ya kuipata Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi. Tulitaka CHASO itoe mchango zaidi. Msukumo ambao tulijaribu kuutoa ulipata upinzani wa ndani.”

1 Comment

  • Nakumbuka Zitto Kabwe alisema ACT – Wazalendo kinapigania Tume Huru. Naye Naye Freeman Mbowe akasema CHADEMA kinapigania Katiba Mpya.
    Sidhani mgongano wa CHASO ni baina ya maslahi ya ndani dhidi ya maslahi ya nje.
    Serikali ya wanafunzi inafanya nini?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!