Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wafanyabiashara kortini kwa kuisababishia Serikali hasara Bil 10.5
Habari Mchanganyiko

Wafanyabiashara kortini kwa kuisababishia Serikali hasara Bil 10.5

Spread the love

 

WAFANYABIASHARA watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa 13 yakiwamo kukwepa kodi iliyopelekea Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupata hasara ya Sh. 10.5 bilioni. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea). 

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo jana tarehe 24 Juni 2022, ambapo Wakili wa Serikali Mwandamizi kutoka TRA, Medalakini Emmanuel amesoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Ramadhani Rugemalira.

Washtakiwa kwenye shauri hilo ni pamoja na Joseph Msaki, (35), Gifti Msaki (40) na Constantino Romani (38) wote wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Ramadhani Rugemalira amedai washtakiwa wametenda makosa hayo kati ya Januari 2018 na Juni 15,2022 jijini Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka manne ya kukwepa kodi, mashtaka manne ya kutoa risiti zisizo halali za mashine ya EFD, mashtaka manne ya matumizi yasiyo sahihi ya mashine ya EFD na pamoja na shtaka moja la kuisababishia TRA hasara.

Katika shtaka kukwepa kodi washtakiwa hao wanadaiwa kati ya Januari, 2018 hadi Juni 15, 2022 jijini Dar es Salaam washtakiwa kwa pamoja wakiwa na nia ovu walijihusisha na kutoa risiti isiyo halali kwa kutumia mashine ya EFD iliyosajiliwa kwa jina la Romani Shirima ambayo kwenye taarifa ilikuwa na mauzo ya Sh 18,668,611,770 na kusababisha ukwepaji kodi wa ongezeko la thamani ya Sh. 5,580,002,499.

Pia washtakiwa hao wanadaiwa kutumia mashine ya EFD iliyosajiliwa Kwa jina la Ahmada Ally na kusababisha ukwepaji kodi wa Sh. 784,734,295 huku mashine hiyo hiyo ikitumika tena kusababisha ukwepaji wa kodi ya Sh. 582,551,181.

Katika shtaka la kutoa risiti isiyo sahihi inadaiwa katika kipindi hicho washtakiwa walitoa risiti isiyo sahihi kwa kutumia mashine ya EFD iliyosajiliwa kwa jina la Ahmada Ally wakati mashine hiyo ilikuwa na taarifa ya mauzo ya Sh. 2,622,040,982 na kusababisha ukwepaji kodi wa Sh. 784,734,295.

Katika shtaka la matumizi yasiyo sahihi ya mashine ya EFD inadaiwa, kwa pamoja washtakiwa walitumia mashine hiyo isiyo sahihi yenye jina la Ngarasoni Shirima ambayo ilikuwa na mauzo ya Sh.18,668,611,770 kwa nia ya kumdanganya Kamishna Mkuu wa TRA na kusababisha ukwepaji Kodi ya ongezeko la thamani ya Sh 5,580,002,499

Katika shtaka la kuisababishia TRA hasara inadaiwa, katika kipindi cha Januari 2018 na Juni 15, 2022 washtakiwa hao kwa pamoja huku wakiwa na nia ovu ya kukwepa kodi waliisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh. 10,507,755,190.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Kesi hiyo imeahairishwa hadi Julai 8, 2022 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!