Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge, Serikali zatofautiana kuhusu kukopa ndani
Habari za Siasa

Bunge, Serikali zatofautiana kuhusu kukopa ndani

Ukumbi wa Bunge
Spread the love

 

WAKATI Kamati ya Bunge ya Bajeti ikiishauri Serikali kupunguza kukopa katika soko la ndani ili kuipa nafasi sekta binafsi kukopa, yenyewe imeongeza kiasi inachotarajia kukopa mwaka ujao wa fedha ikilinganishwa na kiasi ilichokopa mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Katika mwaka wa fedha 2021/22 Serikali ilikusudia kukopa jumla ya Sh4.99 trilioni na hadi kufikia mwezi Aprili 2022 mikopo kutoka vyanzo vya ndani ilifikia Sh. 4.12 trilioni sawa na asilimia 82.57 ya lengo.

Kutokana na hali hiyo kamati leo Alhamisi tarehe 16 Juni, 2022, imeishauri Serikali kupunguza kukopa ndani “ili kuipa nafasi sekta binafsi kupata mikopo kwa riba nafuu ili kuchochea uwekezaji na hatimaye kukuza uchumi wa nchi.”

Mbali na ushauri huo wa Kamati, Serikali imeongeza zaidi makadirio ya kukopa katika soko la ndani kutoka Sh 4.99 mwaka 2021/22 hadi Sh 5.78 trilioni mwaka 2022/23.

Kati ya kiasi kinachotarajiwa kukopwa na Serikali Sh3.30 trilioni ni kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za Serikali zinazoiva na kiasi cha Sh2.48 trilioni ni kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!