VIKOSI vya Jeshi la Kanda ya Afrika Mashariki, vinatarajiwa kutumwa mara moja katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama mashariki mwa taifa hilo. Unaripoti Mtandao wa BBC … (endelea).
Hatua hiyo inakuja kufuatia wito wa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, kwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo, uliotaka kikosi cha Kanda ya Afrika Mashariki kwenda Congo kwa ajili ya kurejesha usalama katika mikoa ya Ituri, Kivu Kaskazini na Kusini.
Mbali na wito huo, Rais Kenyatta ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) amevita vikundi hasimu kuacha mara moja mapigano bila masharti yoyote.
Rai hiyo ya Rais Kenyatta umetolewa baadaya hivi karibuni mapigano kati ya vikundi vya waasi na Jeshi la Congo, kupamba moto.
Vikosi vya kijeshi vya Kanda ya Afrika Mashariki, vitakwenda kuungana na vikosi vya Umoja wa Mataifa (MUNOSCO).
Leave a comment