Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT Wazalendo waitaka Serikali imrejee U-wakili Fatma Karume
Habari za Siasa

ACT Wazalendo waitaka Serikali imrejee U-wakili Fatma Karume

Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo akizungumza na wanachana wa chama hicho katika jimbo la Nyasa mkoani Ruvuma.
Spread the love

 

CHAMA cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kutekeleza wa ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kufungua ukurasa mpya wa kisiasa kwa kumrejeshea uwakili mwanaharakati machachari Fatma Karume. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ruvuma … (endelea).

Wito huo imetolewa jana tarehe 14 Juni, 2022 na Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu kwenye kikao cha viongozi na wanachama wa Kata ya Lilambo, jimbo la Songea Mjini mkoani Ruvuma.

Wakili Fatma Karume alifutiwa uwakili wake Mwaka 2019 kutokana na kesi ambayo ilifunguliwa na Shaibu wakati huo akiwa Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo dhidi ya Rais John Magufuli kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Adeladus Kilangi (Miscellaneous Civil Cause No. 29 of 2018).

Amesema baada ya kuapishwa, Rais Samia aliahidi kufungua ukurasa mpya wa kisiasa nchini na ameanza kuchukua baadhi ya hatua ikiwemo kufanya mazungumzo na viongozi wa vyama vya upinzani.

“Bila shaka, kwenu nyinyi wakazi wa Lilambo hatua hii ni jambo lenye maana sana. Ninafahamu hapa Lilambo diwani wa ACT Wazalendo, Philipo Mhagama alishinda kwa matokeo ya vituoni lakini hakutangazwa.

“Ninawapongeza kwa mapambano yenu na hatua mlizochukua kupigania haki ikiwemo kulima vibarua mashambani ili kumchangia fedha afungue kesi kupinga matokeo. Hongereni sana” amesema Shaibu.

Hata hivyo, amesema dhana ya kufungua ukurasa mpya nchini inapaswa kutanuliwa na kuwagusa wahanga wote wa utawala uliopita.

Pia inapaswa kuwagusa wavuvi waliochomewa nyavu zao, wakulima walioporwa korosho zao, wafanyabiashara walioporwa mitaji yao, wanaharakati na viongozi waliofungwa au kupotea, amesema Katibu Mkuu huyo.

“Leo nina ombi maalum kwa Serikali. Ninaomba imrejeshee Wakili Fatma Karume uwakili wake. Bila kuathiri taratibu za kimahakama, nina hakika, hatua ya kumfutia uwakili wake ilitokana na msukumo wa kisiasa ili kumuadhibu kwa kesi aliyoisimamia kwa niaba yangu dhidi ya Rais Magufuli. Kama sehemu ya kufungua ukurasa mpya, naye apewe nafasi ya kuendelea na majukumu yake ya uwakili” amesema Shaibu.

Katibu Mkuu huyo anaendelea na ziara ya siku sita kwenye majimbo mbalimbali ya mkoa wa Ruvuma ambayo itahitimishwa tarehe 17 Juni mwaka huu.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!