Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wizara ya fedha waomba bajeti Sh trilioni 14
Habari za Siasa

Wizara ya fedha waomba bajeti Sh trilioni 14

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango
Spread the love

 

WIZARA ya Fedha na Mipango, imeliomba Bunge lipitishe bajeti ya Sh. 14.94 trilioni, kwa ajili ya matumizi yake katika mwaka wa fedha wa 2022/23, huku likitaja vipaumbele vyake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hoja hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 7 Juni 2022, bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa fedha.

Waziri huyo wa fedha amesema, kati ya fedha hizo, Sh. 13.62 trilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, wakati Sh. 1.32 trilioni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

“Wizara ya Fedha na Mipango inawasilisha mbele ya Bunge lako tukufu, maombi ya kuidhinishiwa jumla ya Sh. 14.94 trilioni,” amesema Dk. Mwigulu.

Dk. Mwigulu amesema, Wizara ya Fedha imeomba kuidhinishiwa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele mbalimbali, kwa kuzingatia malengo, shabaha na vipaumbele vilivyoidhinishwa katika Mpango wa Matumizi wa Muda wa Kati (MTEF) na Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano (2021/22-2025/26).

“Vipaumbele vya wizara ni kukusanya, kutafuta na kudhibiti mapato na matumizi ya Serikali. Kuhudumia kwa wakati deni la Serikali pindi linapoiva, kufanya tathimini ya dira ya taifa ya maendeleo 2025, kufanya tathimini ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo,” amesema DK. Mwigulu.

Dk. Mwigulu amesema “kurejesha bahati nasibu ya taifa na kufanya utafiti katika sekta za uzalishaji ili kuibua fursa za uwekezaji, uwezeshaji na vyanzo vya mapato ya Serikali katika muda mfupi, kati na mrefu. Kutekeleza maagizo ya Serikali kutafsiri Sgeria za wizara na tasisi zake kwa lugha ya Kiswahili na kuhuisha mwongozo wa taifa wa usimamizi viashiria hatarishi.”

Wakati huo huo, Dk. Mwigulu ametaja maeneo ambayo fedha hizo zitakwenda kutumika, ikiwemo, uimarishaji usimamizi mifumo ya usimamizi wa fedha za umma kupitia program ya maboresho ya usimamizi wa fedha za umma awamu ya sita, kuandaa na kujenga ghala la takwimu. Kuratibu na kusimamia zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.

“Maeneo mengine kuziwezesha taasisi za wizara hususan taasisi za elimu na mafunzo kuboresha miundombinu ya kujifunza na kufundishia. kuendelea na ujenzi wa jengo la wizara katika mji wa Magufuli, Mtumba Dodoma,” amesema Dk. Mwigulu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!