Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Tangulizi Mbunge: Dk. Mwigulu unafeli wapi? futa leseni hizi
Tangulizi

Mbunge: Dk. Mwigulu unafeli wapi? futa leseni hizi

Dk. Mwigulu Nchemba
Spread the love

MBUNGE wa Mbogwe, Nicodemas Maganga (CCM) leo Jumanne amemtaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba kutumia mamlaka aliyonayo kuzifutia leseni benki ambazo zimegoma kuwapunguzia riba wafanyabiashara wa ndani waliokopa kipindi cha janga la maambukizi ya Corona. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Amesema licha ya Rais wa awamu ya Tano, Dk. John Magufuli na awamu ya sita, Samia Suluhu Hassan kuagiza riba ipunguzwe, bado asilimia kubwa ya benki nchini zimegoma kutekeleza agizo hilo.

Akichangia makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa fedha 2022/2023 leo tarehe 7 Juni bungeni jijini Dodoma, Maganga amesema benki za ndani zinawakanyaga wafanyabiashara wa ndani.

“Hotuba ya Rais wa awamu ya tano, aliagiza riba zipungue kwenye haya mabenki, pia Rais wa awamu ya sita wakati anahutubia Bunge, suala la riba aliagiza zipungue. Waziri hizi taasisi zipo chini yako… unafeli wapi wakati una mamlaka ya kufuta hata leseni za hizi benki,” amesema Maganga na kuongeza;

“Wanasiasa wengi wanasimama wanasema nchi imefunguliwa lakini kufunguliwa huku kunaweza kuwa maumivu kwetu kwa sababu kama sisi wa ndani tunapigwa riba za juu, alafu mgeni akija anapoozewa riba nchi imefunguliwaje? labda wamefunguliwa wa nje.”

Pamoja na kumuomba Waziri huyo alichukulia suala hilo kwa umakini, pia Mbunge huyo alidai kuwa taasisi hizo za kifedha hazina kauli nzuri kwa wafanyabiashara wa ndani.

Amesema taasisi nyingi haziwavumilii wafanyabiashara.

“Kwa mfano mtu amerejesha marejesho tisa bado matatu, unaenda kukamata nyumba yake, unaenda kumfilisi. Ina maaa unampa mkopo kwa lengo la kumfilisi?

Pamoja na mambo mengine amesema hali halisi ya maisha ya Watanzania si kweli kwamba kuna unafuu kwani bado hali ni ngumu.

“Angalia kama kuna sehemu yoyote fungulia pesa ili zijae mifukoni kwa wanyonge maana kwenye kampeni huwa tunasema tunawapigania wanyonge sasa hawajapata pesa bado,” amesema.

Pia alimshauri Dk. Nchemba kwamba wizara yake iandae mpango wa mafunzo kwa vijana wanaoajiri na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kabla ya kwenda kwa wafanyabiashara kudai kodi ili watumie kauli nzuri ili kuwafanya watu walipe kwa hiari.

Mbunge wa Mbogwe, Nicodemas Maganga (CCM)

Aidha, akijibu hoja hizo katika majumuisho ya makadirio ya bajetio yake, Dk. Nchemba amesema kuhusu suala la riba Serrikali inaendelea kulifanyia kazi.

“Tunachotumia kwenye riba tunatumia nguvu ya soko kuamua masuala ya kiuchumi, majirani zetu walitumia nguvu ya dola kuweka ukomo kwamba asubuhi tunaamka na kusema riba asilimia tano, ikaleta madhara kiuchumi.

“Unaweza kukiathiri kimoja vikaleta viashiria kwingine, hili linakwenda likitekelezeka naamini litakwenda kufanyika vizuri,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema: Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!