Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari Chama ‘Magufuli’ moto, mawaziri nawabunge wahusishwa kujiunga
HabariTangulizi

Chama ‘Magufuli’ moto, mawaziri nawabunge wahusishwa kujiunga

Spread the love

 

CHAMA kipya cha siasa nchini Tanzania kinachojinasibisha na ‘Rais wa Wanyonge’, John Magufuli, kimeanza kuleta sintofahamu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya baadhi ya viongozi wake, wakiwamo wabunge na waliokuwa mawaziri, kuhusishwa nacho. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa ndani ya chama tawala-CCM zinasema, hofu ya baadhi ya viongozi kuhusu ujio wa chama hicho kipya cha Umma Party (UP), ni kutokana na hofu kuwa baadhi ya wanaokiunga mkono, ni waliokuwa wasaidizi wa karibu na Rais Magufuli.

Umma Party kilizinduliwa juzi Jumapili, Manzese, jijini Dar es Salaam, huku viongozi wake wakiwa wamevalia fulana zenye picha ya Rais Magufuli, huku kwenye mitandao ya kijamii, mjadala mkubwa ukiwa ni uundwaji wa chama hicho.

Haya yanatokea, zikiwa zimesalia takribani miaka mitatu kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, huku chama hicho kikiendelea kutafuta wadhamini ili kupata usajili wa kudumu.

Taarifa zinahusishwa na chama hicho na minong’ono kuwa miongoni mwa waasisi wake, ni vigogo walioko CCM na Upinzani.

Undani wa habari hii, soma Gazeti la Raia Mwema la leo Jumanne tarehe 19 Aprili 2022 kujua alichosema mwenyekiti wake, Seif Maalim Seif na mengine mengi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!