Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NEC yajitetea madudu uchaguzi 2020
Habari za Siasa

NEC yajitetea madudu uchaguzi 2020

Spread the love

MKURUGENZI wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Wilson Mahera, amesema dosari zinazojitokeza katika chaguzi, zinasababishwa na watumishi wanaoajiriwa kwa muda, kutopata mafunzo ya kutosha ya usimamizi wa mchakato huo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Dk. Mahera ametaja sababu hiyo leo Jumanne, tarehe 5 Aprili 2022, katika kongamano la haki, amani na maridhiano, lililofanyika jijini Dodoma, baaba ya washiriki wake kutoa malalamiko kuhusu dosari zilizojitokeza katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Mkurugenzi huyo wa uchaguzi NEC, amesema tume hiyo ina wajumbe saba na watumishi walioajiriwa 200, lakini inapokwenda kwenye uchaguzi huajiri kwa muda watu zaidi ya 400,000 kwa ajili ya kusimamia mchakato wa uchaguzi.

“Zile siku chache za uchaguzi tunatoa training siku nne au tatu, wafuate hayo maagizo ambayo tunatoa kwa wasimamizi wa uchaguzi, watendaji ngazi za vituo na kwa vyama vya siasa. Watu kama hao wameoata semina siku mbili,” amesema Dk. Mahera.

Dk. Mahera amesema “kwa mfumo ambao tunaona kama mmoja mmoja akitenda kosa kule, linageuzwa kuwa kosa la wajumbe wa tume. Wajumbe wa tume sana watatembea mpaka huko saa ngapi kwenda kuiba kura? Kwa hiyo naweza jikuta kuna tatizo kashindwa kutatua,”

Dk. Mahera amesema sababu nyingine zinazopelekea chaguzi kuwa na malalamiko, ni ukata wa fedha kwa vyama vya siasa kuendeshea kampeni na kulipia mawakala kwa ajili ya kulinda kura zao.

“Nyie mnajuana wanasiasa kama huwezi kulipia mawakala wako na vyama vingine vina fedha, vinaweza kulipia mawakala wake, wanaweza kukubaliana huko,” amesema Dk. Mahera.

Katika hatua nyingine, Dk. Mahera amesema changamoto ya wagombea wa Uchaguzi 2020, hasa wa wabunge kutoshiriki uchaguzi huo kwa sababu ya kuenguliwa katika mchakato wa uteuzi, imesababishwa na wahusika kutokata rufaa NEC.

Amesema, kama wagombea hao wangetaka rufaa NEC wangerudishwa kugombea.

Dk. Mahera amesema, NEC ilipokea malalamiko kwa ngazi ya wagombea ubunge 2,000 walioenguliwa, lakini waliokata rufaa katika ngazi ya jimbo ni 165, ambapo 98 kati yao walienguliwa. Majina hayo yalipitiwa kisha 131 walirudishwa kugombea.

“Kwa hiyo katika 165, 131 walirudi kwenye orodha ya wagombea ubunge. Kwa hiyo unaona kama wale wangeacha kufuata sheria wakabaki huko, ina maana wabunge 131 wasingeweza kushiriki,” amesema Dk. Mahera.

Dk. Mahera amevitaka vyama vya siasa kutoa mapendekezo yao juu ya ufumbuzi wa dosari hizo.

“Kama mnaona kuna changamoto za sheria za uchaguzi, zinazohusiana na masuala ya uchaguzi, zinazotoa mwanya watu kukatwa huko chini, kuonewa, kutoruhusiwa kuingia vituoni, mnayo fursa ya kuangalia changamoto kama hizo zikarekebishwa,” amesema Dk. Mahera.

Dk. Mahera amesema, tume za uchaguzi za nchi za Afrika zinakabiliwa na chnagamoto mbalimbali.

“Lakini tume za taifa za uchaguzi zimekuwa zina changamoto nyingi tu, si ya kwetu. Zimekuwa zikilaumiwa sana kuhusiana na masuala ya uteuzi wa wajumbe, kwa hiyo kumekuwa na changamoto za kutokuamini sababu wajumbe wake wanateuliwa na Rais, hawaamini kama wnaaweza kufanya kazi bila kupendelea,” amesema Dk. Mahera.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

error: Content is protected !!