May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba vitani tena na wasauzi Robo fainali ya shirikisho Afrika

Spread the love

 

Klabu ya soka ya Simba Tanzania imepangiwa kukutana na Orlando Pirates ya nchini Afrika kusini katika robo fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika mara baada ya kuchezeshwa droo. Anaripoti Damas Ndelema Tudarco (endelea)

Droo hiyo imechezeshwa hii leo tarehe 5 Aprili 2022, jijini Cairo nchini Misri yalipo makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika ‘CAF’

Simba imefika hatua hiyo ya robo fainali baada kufanikiwa kukusanya jumla ya pointi kumi na kumaliza nafasi ya pili katika group D wakiwa na pointi 10, sawa na RS Berkane waliokuwa kwenye nafasi ya kwanza.

Mchezo wa kwanza wa hatua hiyo utapigwa Aprili 17 kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, huku mchezo wa marudiano ukipigwa wiki moja mbeleni tarehe 24 Aprili 2022, Soweto nchini Afrika Kusini.

Hii itakua mara ya pili kwa Simba kupangiwa timu kutoka Afrika Kusini baada ya msimu uliopita kupangiwa kucheza na Kaizer Chief katika hatua kama hii ya robo fainali kwenye michuano ya klabu bigwa na Simba kuondoshwa kwa katika hatua hiyo kwa jumla ya mabao 4-3.

Aidha mshindi kati ya Simba na Oralndo Pirets ata kutana na mshindi war obo fainali ya pili kati ya Al Ahl Tripoli dhidi ya Al ltthad Sc.

error: Content is protected !!