Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Ukraine aitisha maandamano duniani kupinga Urusi
Kimataifa

Rais Ukraine aitisha maandamano duniani kupinga Urusi

Spread the love

RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelensky ametoa wito kwa watu duniani kote kuandamana barabarani kama hatua ya kupinga uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Aidha, akihutubia bunge la Ufaransa, Rais huyo ametumia fursa hiyo kuzitaka kampuni za Ufaransa ambazo bado zinaendesha oparesheni zake nchini Urusi, kuacha kufadhili harakati zinazofanywa na Urusi nchini Ukraine. Anaripoti Mwandishi wetu … (endelea).

Katika ujumbe wake wa dakika 15, alioutoa jana tarehe 23 Machi, 2022 Zelensky aliyekuwa amevaa fulana ya rangi ya kijani kibichi ameonekana kuwasuta watu wanaofaidika kifedha na vita hivyo.

Rais huyo wa Ukraine alizitaja kampuni ya magari ya Ufaransa ya Renault, Auchan na kampuni ya mapambo ya nyumba na samani ya Leroy Merlin akizitaka kuacha kuifadhili Urusi inayotumia fedha hizo kumwaga damu za watu wa Ukraine.

Aidha, Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba alikwenda mbali zaidi kwa kutoa wito wa kususiwa kwa kampuni kongwe ya Renault, inayosifika barani Ulaya kwa utengenezaji wa magari.

Pamoja na mambo mengine wabunge wa Ufaransa waliipongeza hotuba ya Zelenksy, ambaye amekuwa akizungumza na mabunge mbalimbali ya Ulaya ili kutafuta uungwaji mkono.

Uwepo wa zaidi ya kampuni 500 za Ufaransa nchini Urusi kumezua mjadala mpana nchini Ufaransa, katikati ya shinikizo ya kuzitaka kampuni hizo zijiunge na kampuni nyengine za Marekani na Uingereza kukata uhusiano na Urusi.

Tayari kampuni za McDonald, Apple na BP zimesitisha oparesheni zake nchini Urusi.

Hata hivyo, hakuna kampuni yoyote ya Ufaransa iliyofunga matawi yake nchini Urusi.

Katika ujumbe alioutoa kuelekea mkesha wa kumbukumbu ya mwezi mmoja wa uvamizi wa Urusi, Zelensky amewataka watu duniani kote kusimama imara dhidi ya Urusi na kupinga vita hivyo.

Rais huyo wa Ukraine pia ametoa wito kwa muungano wa jeshi la kujihami la NATO kuipa msaada Ukraine ikiwemo wa silaha ili kupambana na wanajeshi wa Urusi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!