Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kamati ya Bunge yampongeza Rais Samia
Habari Mchanganyiko

Kamati ya Bunge yampongeza Rais Samia

Spread the love

KAMATI ya Bunge ya Miundombinu imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuendeleza mradi wa ujenzi meli ya MV Mwanza ili kurahisisha usafiri na usafirishaji katika mikoa inayozunguka Ziwa Viktoria na nchi jirani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza baada ya kukagua na kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo jijini Mwanza, Mwenyekiti Seleman Kakoso amesema Serikali ya Awamu ya tano imeendelea kutoka fedha ili kuendeleza mradi huo ambapo dhamira hiyo itakuza pato la mkoa na Serikali baada ya mradi kukamilika.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Atupele Mwakibete akifafanua jambo kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miudombinu, wakati kamati hiyo ilipotembelea Mradi wa MV Mwanza, jijini Mwanza.

“Naipongeza Serikali sababu taarifa tuliyopewa hapa ni kuwa Mkandarasi ameshalipwa Certificate zote alizowasilisha kilichobaki ni sisi kama watanzania kujiweka tayari kwa meli hiyo itakapokamilika,” amesema Mwenyekiti Kakoso.

Mwenyekiti Kakoso ameeleza umuhimu wa kuzingatia mahitaji ya rasilimali watu hasa kwenye taasisi zenye miradi mikubwa na kusisitiza kuwa uwepo wa watumishi wa kutosha kwenye kada muhimu kama uhandisi na manunuzi kwamba kutaongeza tija na uzoefu kuanzia mwanzo wa miradi mpaka uendeshaji wa miradi inapokamilika.

Aidha, Mwenyekiti Kakoso ameitaka Wizara kusimamia Taasisi zinazofanya kazi kwa karibu ikiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Kampuni ya Huduma Meli (MSCL) na Shirika la Reli ya Tanzania (TRC) ili kuhakikisha mipango ya taasisi hizo inakwenda pamoja ili kuepuka kupishana kwenye utekelezaji wa miradi.

Naye Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete, amemuhakikishia Mwenyekiti wa Kamati hiyo na wajumbe kuwa tayari Serikali imeshatoa maelekezo kwa taasisi hizo kushirikiana ili miradi itakapokamilika kusiwe na visingizio kwenye uendeshaji.

Naibu Waziri Mwakibete ameeleza kuwa pamoja na juhudi mbalimbali zinazoendelea tayari Kampuni ya Huduma za Meli, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Shirika la Reli Tanzania (TRC) zimeshatiliana saini makubaliano maalum ya kusafirisha mizigo ikiwa ni moja ya jitihada ya ushirikiano.

Kamati ya Miundombinu iko Mkoani Mwanza kuakagua miradi ya WIzara ya Ujenzi na Uchukuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!