Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Muarobaini wakazi Kivulini kutembelea KM 65 kusaka huduma za afya wapatikana
AfyaHabari Mchanganyiko

Muarobaini wakazi Kivulini kutembelea KM 65 kusaka huduma za afya wapatikana

Spread the love

HATIMAYE kilio cha wakazi wa Kata ya Kivulini Manispaa ya Lindi, mkoani Lindi kuhusu upatikanaji wa huduma za afya, kimepata suluhu baada ya ujenzi wa Kituo cha afya Kivulini kuanza. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Wakazi hao ambao walikuwa wakitembea umbali wa kilomita 65 kufuata huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa ya Sokoine, wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuikumbuka kata hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti hivi karibuni, wakazi hao walianza kueleza machungu waliyoyaonja kabla ya ujio wa kituo hicho cha afya.

Mmoja wa wakazi hao, Hadija Nampamba amesema mwaka 2000 almanusura ampoteze mdogo wake aliyekwenda kujifungua katika Hospitali ya Sokoine na kumpoteza mtoto.

Amesema awali walikwenda katika Zahanati moja iliyopo kijijini hapo lakini wakapewa rufaa kuelekea Hospitali ya Sokoine ambapo walimpandisha mjamzito huyo katika machela kisha wakatumia baiskeli kumfikisha hospitali hapo.

“Baada ya kufika awali walitaka kumfanyia upasuaji lakini baadae wakashauri aongezewe chupa nne za maji ya uchungu, ambapo baada ya saa nne alijifungua lakini mtoto alipoteza maisha na mama akapoteza fahamu.

“Kwa kweli kama kituo hiki cha afya kingekuwepo naamini mtoto wetu angekuwepo,” amesema.

Aidha, mkazi mwingine wa kijiji cha Maloo, Katibule Abdalah mbali na kumshukuru Rais Samia kwa kuelekeza ujenzi wa kituo hicho, alimuomba aongeze kituo kingine ili kumaliza tatizo la huduma za afya katika kata hiyo.

RC LINDI

“Ninamuombea Mwenyezi Mungu amuweke salama kwa sababu wakazi wa kata hizi tulikuwa nyuma sana. Tunamuoma atuongezee na nyingine,” amesema.

Aidha, Mkuu wa mkoa wa Lindi, Zainab Telack amesema umbali huo wa kilomita 65 ulikuwa ni kielelezo tosha kwamba hapa kulikuwa kunahitaji huduma ya afya.

“Huko tulikokwenda kujenga kote tathmini imefanywa watu waliopo na mahitaji,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza namna Nathwani alivyomjeruhi jirani yake

Spread the loveMSIMAMIZI wa Msikiti wa Wahindi Lohana aitwae, Ankit Dawda (32)...

error: Content is protected !!