Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe ataja chanzo cha kukamatwa, kufunguliwa kesi ya ugaidi
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe ataja chanzo cha kukamatwa, kufunguliwa kesi ya ugaidi

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama cha Chadema, Freeman Mbowe, amedai chanzo cha yeye kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi, ni hotuba yake ya uchambuzi wa utawala wa Serikali ya awamu ya tano iliyokuwa ikiongozwa na Hayati John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa … (endelea).

Mbowe ametoa madai hayo leo Jumanne, tarehe 8 Machi 2022, mkoani Iringa akizungumza katika kongamano la maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, lililoandaliwa na Baraza la Wanawake la Chadema (BAWACHA).

Hotuba hiyo ilitolewa na Mbowe tarehe 21 Aprili 2021, takribani mwezi mmoja tangu Rais Magufuli afariki dunia. Alikamatwa na Jeshi la Polisi akiwa mkoani Mwanza, tarehe 21 Julai mwaka 2022.

“Mtakumbuka tarehe 21 Aprili 2021 nilizungumza nanyi katika hotuba ambayo wengi wanapenda kuita ya never and never again, ambayo pia inapatikana kwenye mtandao wa youtube. Katika hotuba ile nilichambua kwa kina hali ya nchi yetu ilivyokuwa kwenye utawala awamu ya tano,” amesema Mbowe.

Mwanasiasa huyo amedai, hotuba ile haikuwapendeza baadhi ya watu waliokuwa madarakani.

“Uchambuzi ule uligusa wengine wakahisi hasi, zaidi wale waliokuwa madarakani katika utawala wa awamu ya tano na wengine bado wako mpaka leo. Chukizo zito lilijengwa dhidi yangu. Kusema ukweli haikuwapendeza wenye mamlaka, miezi mitatu kamili bada ya hotuba yangu ile nilitiwa nguvuni ndio nimetoka siku nne zilizopita,” amesema Mbowe.

Mwenyekiti huyo wa Chadema, kauli yake iliyowataka Watanzania wasikubali madhila yaliyojitokeza katika awamu hiyo yasijirudie, ndiyo sababu ya kukaa mahabusu kwa zaidi ya miezi saba.

“Binafsi nina amini nilichopitia safari hii kimechagizwa kwa kiasi kikubwa na hotuba ile ya uchambuzi wa Serikali ya awamu ya tano na dhambi walizofanyiwa Watanzania na kauli yangu tukatae jambo hili never and never again, kuruhusu mtu yeyote wa chama chochote kulifanya Taifa kuwala maombolezo,” amesema Mbowe.

Mbowe amesema “kiongozi wa chama cha siasa kama nafasi yangu kuna wakati unalazimika kufanya maamuzi magumu sana na mara zote ukifanya maamuzi bila kujiamini na kwa hofu, bila dhamiri ya roho yako lazima utakwamia njiani ndugu zangu Watanzania.”

Mbowe amesema licha ya kupitia madhila hayo, Chadema hakitaacha kusema ukweli kuhusu mambo yanayoendelea nchini.

Mbowe alikuwa anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 16/2021, iliyokuwa na walinzi wake, Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya, kwenye Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo iliyoondolewa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu, tarehe 4 Machi 2022, Mbowe na wenzake, walidaiwa kupanga njama za kutaka kuwadhuru viongozi wa Serikali, kufanya maandamano nchi nzima na kulipua vituo vya mafuta na maeneo yenye mikusanyiko ya watu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!