Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Putin aonya vikwazo zaidi dhidi ya Urusi
Kimataifa

Putin aonya vikwazo zaidi dhidi ya Urusi

Spread the love

 

RAIS Putin ametoa onyo kwa wale wanaopinga hatua ya Urusi nchini Ukraine “kutozidisha tatizo kuwa baya zaidi” kwa kuiwekea nchi yake vikwazo zaidi. Inaripoti BBC … (endelea).

Rais wa Urusi alikuwa akizungumza katika mkutano wa serikali uliotangazwa kwenye kituo cha habari cha Rossiya 24 kinachomilikiwa na serikali.

“Hatuna nia mbaya dhidi ya majirani zetu,” Putin amedai.

Na anasema serikali yake haioni ” haja” kwa majirani zake kuchukua hatua zaidi ambazo “zitafanya uhusiano wao kuwa mbaya zaidi”.

“Nadhani kila mtu lazima afikirie jinsi ya kurekebisha uhusiano, kushirikiana kawaida na kukuza uhusiano kama kawaida,” ameongeza.

Haya yanajiri wakati mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi za Magharibi wakikusanyika mjini Brussels kutafakari jinsi ya kuishinikiza Urusi kusitisha vita.

Putin pia anarudia madai yake ya awali kwamba hatua zote zilizochukuliwa na jeshi la Urusi hadi sasa zimefanywa “pekee katika kukabiliana na baadhi ya hatua zisizo za kirafiki dhidi ya Urusi”.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!