Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Balozi Mbarouk amuaga balozi wa Vatican
Tangulizi

Balozi Mbarouk amuaga balozi wa Vatican

Spread the love

NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amekutana na kumuaga Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Marek Solczyński baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza wakati wa kumuaga Balozi wa Vatican jana tarehe 22 Februari, 2022 katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam, Balozi Mbarouk amempongeza Balozi Solczyński kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kudumisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na Tanzania.

Pamoja na mambo mengine, Balozi Mbarouk amemuahidi Askofu Mkuu Solczyński kuwa Tanzania na Vatican zitaendelea kuhimiza amani na utulivu katika masuala yenye changamoto mbalimbali ili kuwezesha uwepo wa amani na kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Baba Mtakatifu katika kulinda amani na usalama duniani kote.

Kwa upande wake Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu Marek Solczynski amesema kuwa Vatican itaendelea kuimarisha mahusiano yake ya kidiplomasia na Tanzania kwa masuala yenye maslahi ya amani na utulivu pamoja na haki na utu.

“Tumeongelea masuala mbalimbali katika kukuza diplomasia yetu na tumekubaliana kwa pamoja kudumisha amani na usalama duniani ili kuweza kuchagiza maendeleo endelevu kwa pande zote mbili,” amesema Askofu Mkuu Solczynski.

Balozi wa Vatican nchini Askofu Mkuu Marek Solczyński aliwasili nchini Tanzania Julai 12, 2017.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!