Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Yanga yajikita kileleni, yaibamiza Mtibwa Manungu
Michezo

Yanga yajikita kileleni, yaibamiza Mtibwa Manungu

Spread the love

 

KLABU ya Soka ya Yanga imeendelea kujichimbia kileleni mara baada ya kuibuka na alama tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ulipigwa hii leo Jumatano Tarehe 23 Februari 2022, kwenye dimba la Manungu Complex na Yanga kufanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-0.

Mabao ya Yanga kwenye mchezo huo yaliwekwa kambani na Sadio Ntibanzokiza kwenye dakika ya 45+5, mara baada ya mlinzi wa Mtibwa Sugar kufanya makosa, na Yanga kutumia nafasi hiyo na kufanya bao hilo kudumu mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili kiliporejea, Yanga waliendelea kushambulia na kupelekea kuandika bao la pili kwenye dakika ya 65, likiwekwa kambani na Fiston Mayele.

Bao hilo limekuwa la saba kwa mshambuliaji huyo, toka ajiunge na timu hiyo kwenye dirisha kubwa la usajili mwezi Agosti, akitokea klabu ya AS Vita ya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Yanga.

Mayele kwa sasa anashika nafasi ya pili katika upachikaji mabao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, sawa na George Mpole, ambaye naye amepachika mabao saba mpaka sasa, huku kinara kwenye chati hiyo akiwa Ralient Lusajo wa Namungo FC, ambaye amepachika mabao 10 mpaka sasa.

Kwa ushindi huo Yanga inafikisha jumla ya alama 39, point inane nyuma ya Simba waliokuwa kwenye nafasi ya pili huku wote wakiwa na michezo 15.

Mchezo unakuja Yanga itakuwa nyumbani, kuwakalibisha Kagera Sugar, mchezo utakaopigwa Jumapili ya Tarehe 27 Februari 2022, kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam majira ya saa 1 usiku.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

error: Content is protected !!