Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Ligi Kuu Bara kwenda mapumziko siku 18
Michezo

Ligi Kuu Bara kwenda mapumziko siku 18

Spread the love

LIGI kuu Tanzania Bara imendelea kushika kasi mara baada ya kupigwa michezo 13, huku timu 16 zikionekana kubanana na kwenye msimamo katika kuelekea kumaliza duru la mzunguko wa kwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Katika kuelekea kukamilisha mzunguko wa kwanza, mara baada ya kusalia michechezo miwili, klabu ya Yanga inaonekana kuwa juu ya msimamo ikiwa na alama 25, ikiwa na pointi 35 mara baada ya kucheza michezo 13, ikifuatiwa na Simba kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 25 wote wakiwa na michezo sawa.

Katika msimamo wa Ligi hiyo Yanga ndio klabu pekee kati ya timu 16 zinashiriki Ligi Msimu huu, ambayo imetengeneza wigo mpana wa pointi na mpinzani wake.

Yanga mpaka sasa imemuacha Simba jumla ya alama 10, na timu zote zilizosalia hakuna inayomzidi mpinzani wake anayefuata kwa alama zaidi ya tano.

Ligi hiyo inatarajia kwenda mapumziko ya siku 18, mara baada ya michezo ya mzunguko.wa 14 kuchezwa juma lijalo kupisha kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA kwenye michezo ya kirafiki.

Tayari mpaka sasa baadhi ya wachezaji wa kigeni wa klabu ya Yanga wanaotokea nchini Jamhuri ya Congo akiwemo Juma Shaban na Yanick Bangala wameshajiunga na timu hiyo kwa ajili ya michezo ya kirafiki, kiasi cha kupelekea kukosa mchezo wa kombe le Shirikisho la Azam, ambapo Yanga walishuka dimbani dhidi ya Mbao FC.

Kwenye mchezo huo uliopigwa juzi kwenye dimba la Ccm Kirumba, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, lilowekwa kambani na Fiston Mayele.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!