Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Luteni Urio adai Mbowe hakutaka kuzungumzia ugaidi kwenye simu
Habari za SiasaTangulizi

Luteni Urio adai Mbowe hakutaka kuzungumzia ugaidi kwenye simu

Spread the love

 

SHAHIDI wa 12 wa Jamhuri, Luteni Denis Urio, amedai Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, hakutaka kuzungumzia ugaidi kwenye mawasiliano ya simu, bali alizungumza masuala hayo walipoonana ana kwa ana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Luteni Urio ametoa madai hayo leo Ijumaa, tarehe 28 Januari 2022, akitoa ushahidi wake katika kesi ya uhujumu uchumi, yenye mashtaka ya ugaidi, inayomkabili Mbowe na wenzake, Halfan Bwire Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam, mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

Ni baada ya mawakili wa Mbowe na wenzake, kumbana kuhusu njama za ugaidi anazodaiwa kupanga mwanasiasa huyo, kutoonekana katika mawasiliano yao ya ujumbe mfupi kupitia simu, aliyoyasoma mahakamani hapo.

Wakili wa Utetezi, Dickson Matata, alimuuliza Luteni Urio, kama katika meseji hizo zinazodaiwa kuwa za kwake na Mbowe, kuna mahala zinaonesha Mbowe alipanga kulipua masoko, na mahojiano yao yalikuwa kama ifiatavyo;

Matata: Hiyo meseji inazungumzia kulipua masoko?

Shahidi: Mheshimiwa Jaji suala la kulipua Mbowe hakutaka kuzungumzia kwenye simu au meseji.

Matata: Kuna meseji inaonesha?

Shahidi: Hakuna meseji.

Matata: Kuna sehemu inasema kushambulia viongozi ambao hawapendi upanzani?

Shahidi: Hakuna mahali inasema hivyo.

Matata: Hiyo meseji inasema kulipua vituo vya mafuta?

Shahidi: Hakuna mahali inasema hivyo.

Awali, Wakili Matata alimuuliza Luteni Urio, kama Mbowe akikana kuwa hakuwahi kumueleza mipango yake ya kufanya vitendo vya kigaidi, ana ushahidi wa sauti, meseji au maandishi, utakaothibitisha suala hilo, ambapo alimjibu kama ifuatavyo;

Matata: Mbowe wakati ulipokutana naye, hukona umuhimu wa kuhifadhi voice note (sauti) na meseji?

Shahidi: Sikuwa na device za kuweza kuhifadhi hizo sauti, sikufanya.

Matata: Mbowe akikataa hakukwambia hayo maneno una ushahidi gani wa kuthibitisha?

Shahidi: Ushahidi wa kuthibitisha ni hicho alichoniambia.

Katika ushahidi wake mkuu alioutoa juzi akiongozwa Wakili wa Serikali Mwandamizi, Abdallah Chavula, Luteni Urio alidai mahakamani hapo kuwa, Mbowe alimuelezea mipango yake ya kupanga njama za kufanya vitendo vya ugaidi, alipokutana naye ana kwa ana Julai 2020, maeneo ya Mikocheni, Dar es Salaam.

Alidai kuwa, kabla ya kuonana na Mbowe, mwanasiasa huyo alimpigia simu akimtaka waonane, ambapo alimkatalia na kumuomba azungumze naye kwenye simu, ombi lililokataliwa na Mbowe.

Luteni Urio amedai, baada ya Mbowe kukataa kuzungumza naye kwenye simu, mwanasiasa huyo alimuomba wakutane, ndipo walipokutana akamueleza mipango hiyo.

Shahidi huyo wa Jamhuri anadai kuwa, alipokutana na Mbowe, alimuomba amtafutie makomandoo wa JWTZ, waliofukuzwa kazi au kustaafu, ili wamsaidie katika harakati za chama chake kuchukua dola 2020, kwa gharama yoyote ile.

Ikiwemo kudhuru viongozi wanaonekana kuwa kikwazo kwa vyama vya upinzani. Kulipua vituo vya mafuta na maeneo yenye mikusanyiko ya watu, kufanya maandamano yasiyo na kikomo.

Na kukata miti iliyoko pembezeno mwa barabara kisha kuyapanga magogo katika maeneo hayo, lengo ni kuzua taharuki kwa jamii na kuonesha Serikali imeshindwa.

Luteni Urio pia alisoma meseji anazodai alitumiwa na Mbowe mahakamani hapo, zinazoomesha namna alivyompa maelekezo ya kuwatafuta makomando wa kutekeleza mipango hiyo, lakini pia namna alivyomtumia pesa za kuwaratibu na kuwafikisha kwake jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!