Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mahakama Kuu yaja na mwarobaini wa Mawakili makanjanja
Habari Mchanganyiko

Mahakama Kuu yaja na mwarobaini wa Mawakili makanjanja

Mahakama Kuu ya Tanzania
Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu Tanzania imezindua mfumo wa kuratibu taarifa za mawakili kielektroni (e-wakili) wenye lengo la kudhibiti mawakili wasiotambulika kisheria ‘mawakili makanjanja au vishoka’. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Akifafanua kwa kina kuhusu mfumo huo kwa kina katika Uzinduzi wa nyaraka za mahakama na hamasa ya chanjo ya Uviko -19 leo tarehe 24 Januari, 2022 jijini Dodoma, Msajili Mahakama Kuu, Shamira Sarwat amesema mfumo huo unatambulika kama e – Wakili Management System.

Amesema e-wakili ni mfumo wa kielektroniki ambao umeanzishwa mahsusi kwa ajili ya kusajili, kutunza kumbukumbu na kuratibu leseni za mawakili.

Amesema mfumo huo mpya umejengwa baada ya mfumo wa awali kuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukomo wa teknolojia za kiteknolojia.

“Umejengwa na wataalaam wa ndani na hivyo mahakama inamiliki source codes kwa asilimia 100,” amesema.

Amesema mfumo huo ulioanza kutumika tarehe 5 Januari, 2022 mpaka sasa jumla ya mawakili 10,749 wamesajiliwa na kuongeza kuwa mfumo huo ni zaidi ya daftari la mawakili kwa sababu unabeba taarifa nyingi za mawakili.

Dk Edward Hoseah, Rais wa TLS

“Mfumo huo unakupatia taarifa za wakili kuanzia alipozaliwa, elimu ya msingi, sekondari, vyuo, ofisi yake anakopatikana, namba ya simu na nyingine nyingi.

“Mfumo pia unatoa hudumba mbalimbali kama vile kupokea na kuchakata maombi ya mawakili, kutunza kumbukumbu kwa makundi yao, takwimu za mawakili, kuhuisha leseni za mawakili, malipo ya ada za leseni za mawakili, kutambua uhalali wa leseni ya wakili kuratibu vikao vya kupokea maombi na mawakili,” amesema.

Amesema wananchi wenye kuhitaji huduma za uwakili, wanaweza kutambua mawakili halali na wanaotambulika na mahakama kuu kupitia mfumo huo.

Amesema watumiaji wa mfumo huo ni mawakili wote, waombaji wa uwakili, wananchi, Baraza la Elimu ya Sheria, Ofisi ya msajili mahakama kuu, na Jaji Mkuu.

Ameongeza kuwa hadi sasa mfumo unaendelea kuwa kutoa huduma mbalimbali za kiserikali ikiwamo mfumo wa malipo.

“Tupo katika kuendeleza mfumo huu ili uweze kuwa na mawasiliano ya karibu na wadau muhimu kama NIDA, Law school, Rita na wengine,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!