May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TCRA yamshushia rungu Askofu Mwingira

Askofu wa Kanisa la Efatha, Josephat Mwingira

Spread the love

 

KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imekifungia kipindi cha Efatha Ministries, kinachomilikiwa na Askofu Josephat Mwingira na kurushwa na Star Tv, kwa kosa la kutoa taarifa za zinazozua taharuki, upotoshaji na zinazojenga chuki baina ya wananchi na Serikali. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbali na kukifungia kipindi hicho, kamati hiyo imekionya Kituo cha Televisheni cha Star (Star Tv), huku ikiiamuru kuomba radhi kwa siku tatu mfululizo, kwa kosa la kukubali kurusha taarifa hizo.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu, tarehe 24 Januari 2022 na Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Habbi Gunze, akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

“Star Tv imepewa onyo kali na kutakiwa kuwaomba radhi watazamaji wake kwa siku tatu mfululizo kuanzia kesho hadi Alhamisi, tarehe 27 Januari 2022.  Kipindi cha Efatha Ministries kinasimamishwa kwa muda wa miezi mitatu kuanzia tarehe ya kusoma uamuzi huu,” amesema Ganze.

Ganze amesema, kosa hilo lilitendeka tarehe 26 Desemba 2021, ambapo kipindi hicho kikirushwa mubashara kupitia Star Tv, kilitoa kwa umma taarufa za upotoshaji zisi,o na uthibitishi wowote kuhusu uchaguzi na utendaji wa viongozi wa Serikali na kwamna zimeene,a chuki baina ya Watanzania na viongozi wa Serikali, pamoja na kuleta taharuki miongoni mwa Watanzania.

Aidha, Ganze amesema haki ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo iko wazi ndani ya siku 21 kuanzia leo, katika Baraxa la Ushindani wa Haki Kibiashara (FCT).

Miongoni mwa maudhui yanayodaiwa kutolewa katika kipindi hicho, amnayo yamekiuka kanuni za mawasiliano ya kielektroniki na Posta za 2018, ni ile iliyotolewa na Askofu Mwingira, iliyodai watu watachapana na damu itamwagika kwa sababu wanaibiana kura.

Pia, Askofu Mwingira kupitia kipindi hicho, alitoa kauli iliyodsi shetani mzima mzima yuko Ikulu. Kauli hizo zinadaiwa kukiuka kanuni za utangazaji.

error: Content is protected !!