Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Viongozi, wafuasi 53 Chadema Kakonko mbaroni kisa sherehe za Uhuru
Habari za Siasa

Viongozi, wafuasi 53 Chadema Kakonko mbaroni kisa sherehe za Uhuru

Spread the love

 

VIONGOZI wa Chama cha Chadema wilayani Kakonko, Kigoma takribani 18 na wanachama wao 35, wanadaiwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo, kwa kosa la kukusanyika wakati nchi inasherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).

Taarufa hiyo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 9 Desemba 2021 na Katibu wa Chadema Kanda ya Magharibi, Kangeta Ismail, akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu.

Kangeta amedai kuwa, viongozi hao na wanachama wa Chadema, walikamatwa wakati wanajiandaa kushiriki mkutano wa ndani, uliolenga kusajili wanachama katika mfumo wa kidigitali.

“Tulikuwa na kikao cha ndani cha usajili wanachama katika mfumo wa kidigitali, jana tulimalizia kikao Kibondo,  tukalala Kibondo na asubuhi kuanzia saa 3.00 tilikuwa eneo la Kankono tukiwa njiani tukapata taarifa kuwa Jeshi la Polisi limekata viongozi wasiopoungua 18 na wanachama wasiopungua 35, ambao  wanatoka Jimbo la Bunyungu wilaya ya Kakonko katika,” amedai Kangeta.

Kangeta amedai  kuwa, baada ya kupata taarifa hizo walikwenda katika Kituo chs Polisi Kakonko, kufuatilia suala hilo, anbapo Jeshi la Polisi limesema bado linawahoji wafuasi ha.

“Tulifika kuonana na OCD hoja zao ni zile zile za kila siku wamezuia sababu ya sherehe ya uhuru, sherehe ya uhuru haina msingi watu wasikutane. Siku ya uhuru unaowaondelea watu uhuru,” amedai Kangeta na kuongeza:

“Wametuambia bado hawajachukua maelezo na tuna subiri waachiwe na kikosi chetu kitaendelea sababu hakuna msingi wa kuzuia.”

MwanaHALISI Online imemtafuta Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoms, ACP James Manyama, kwa ajili ya ufafanuzi jui ya tukio hilo, ambaye alisema taarifa hizo hana kwa kuwa yuko safarini. “Sina taarifa kwa kuwa niko safari.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wizara ya Kilimo yapanga kutumia Sh. 1.2 trilioni 2024/25

Spread the loveWIZARA ya Kilimo, imepanga kutumia bajeti ya Sh. 1.2 trilioni...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari za Siasa

Spika Tulia aibana Serikali mafao ya wastaafu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Spread the loveSPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kufanya tathimini...

Habari za Siasa

Serikali yawapa maagizo Ma-RC udhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Spread the loveWAKUU wa mikoa nchini wametakiwa kuandaa utaratibu wa kuwawezesha wananchi...

error: Content is protected !!