Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TAWA yawataka wawekezaji kuchangamkia fursa utalii
Habari Mchanganyiko

TAWA yawataka wawekezaji kuchangamkia fursa utalii

Spread the love

 

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imetoa wito kwa wadau wa utalii kuwekeza katika maeneo ya vitalu 12 vya uwekezaji maalumu (SWICA) ambavyo mwekezaji atamiliki eneo hilo kwa miaka 30. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Wito huo umetolewa jana tarehe 3 Novemba, mwaka huu na Kaimu Kamishna ya Uhifadhi wa Mamlaka ya Wanyamapori nchini (TAWA), Mabula Misungwi katika kongamano la Kampuni za Uwindaji wa Kitalii nchini (TAHOA) lililofanyika jijini Arusha.

Kongamano hilo limelenga kutoa elimu ya uwekezaji mahiri katika maeneo hayo ya vitalu 12 vya uwekezaji maalumu (SWICA) yanayosimamiwa na TAWA.

Misungwi amesema TAWA imeandaa mkakati maalumu wa kuvutia wawekezaji mashuhuri duniani.

Amesema ili kupata fursa ya kuwekeza, kampuni ya mwekezaji mzawa itatakiwa kulipia dola za Marekani milioni 10, kampuni inayomilikiwa na mzawa na mgeni itatakiwa kulipia dola za Marekani milioni 20 wakati mgeni itatakiwa kuwa na mtaji wa dola za Marekani milioni 50.

Aidha, Afisa Mhifadhi – Kitengo cha Huduma za Biashara kutoka TAWA, Said Habibu amewaeleza washiriki wa kongamano hilo kuchangamkia fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana katika maeneo yanayosimamiwa na TAWA.

Ametaja maeneo ambayo yametengwa kwa uwekezaji ni Maswa Mbono, Maswa Kimani na Mkungunero.

Mengine ni pamoja na Ikorongo, Grumeti, Rungwa-Inyonga, Lake Natron (E), Selous LL1, Selous MT2, Selous Ml1, Selous MHN1 na Selous MH12

Katika kikao hicho wadau hao wamesema vikao hivyo vitasaidia kuboresha mambo mbalimbali hususani uwekezaji na uwindaji unaostahili.

Aidha, wadau hao wametoa pongezi kwa elimu hiyo waliyoipata na kuahidi kufanya kazi kwa ukaribu na TAWA.

Katika kikao hicho wadau hao wa utalii walitoa maoni mbalimbali ya namna ya kuboresha SWICA.

Kikao hicho kiliratibiwa na Taasisi ya Serikali inayosimamia sekta binafsi (TPSF) chini ya Mwenyekiti wake Angelina Ngalula.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!