Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Asilimia 75 Dodoma wana uoni hafifu, trakoma! ushirikina watajwa
Habari Mchanganyiko

Asilimia 75 Dodoma wana uoni hafifu, trakoma! ushirikina watajwa

Mgonjwa wa macho akipata vipimo
Spread the love

 

ASILIMIA 75 hadi 85 ya wakazi wa jiji la Dodoma wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ya macho ikiwamo uoni hafifu pamoja na ugonjwa wa trakoma unaonezwa zaidi na inzi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma .. (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 18 Oktoba mwaka huu na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho kutoka katika Hospitali ya Rufaa Dodoma, Dk. Msigalo Erasto wakati akielezea hali ya magonjwa mbalimbali ya macho katika maadhimisho ya wiki ya afya ya macho duniani.

Dk. Erasto amesema mojawapo ya chanzo cha tatizo la uoni hafifu ni matumizi ya simu kwa muda mrefu hususani mwanga wa simu hizo za mkononi, kuangalia televisheni na kompyuta kwa muda mrefu.

Amesema watu wengi wanatatizo la afya ya macho kutokana na mwamko mdogo wa watu kupima afya ya macho mara kwa mara.

Akizungumzia kuhusu Mkoa wa Dodoma, Dk. Erasto amesema wagonjwa wengi wamekuwa wakihusisha matatizo ya macho na imani za kishirikina.

“Tumeona kuwa mkoa wa Dodoma una wagonjwa wengi wa macho na kibaya zaidi wamekuwa wakihusisha ugonjwa wa macho na imani za kishirikina.

“Tunapenda kuhimiza jamii kujitokeza na kujenga desturi ya kupima afya ya macho ili kuhakikisha wanapata matibabu kwa wakati pale wanapogundulika kuwa wanatatizo.

“Katika wiki hii ya maadhimisho ya afya ya macho duniani tunafanya upimaji wa huduma ya macho bure hivyo tunahamasisha jamii kuona umuhimu wa upimaji wa macho na inapotokea tatizo wapatiwa matibabu” ameeleza Dk. Erasto.

Aidha, baadhi ya wananchi wamesema wanakosa huduma hiyo kutokana na vituo vya afya kuwa mbali.

“Elimu ya upimaji wa afya ya macho bado haijaeleweka kwa watu wengi lakini pia huduma zinapatikana kwa tabu, tunachoomba ni serikali kusogeza huduma hiyo karibu na jamii” amesema mmoja wa wananchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

Habari Mchanganyiko

GGML yaja na teknolojia za kisasa maonesho ya OSHA Arusha

Spread the loveKATIKA kuelimisha wananchi na washiriki wa maonesho ya usalama na...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA wawanoa mama lishe 50 kukabiliana na majanga ya moto

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na...

error: Content is protected !!