Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Michezo TFF yawapa ahueni Biashara United
Michezo

TFF yawapa ahueni Biashara United

Spread the love

 

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesongeza mbele mechi kati ya Tanzania Prisons dhida ya Biashara United iliyokuwa ichezwe kesho Jumanne tarehe 19 Oktoba 2021. Anaripoti Damas Ndelema, TUDARCo … (endelea).

Mchezo huo uliokuwa upigwe dimba la Nelson Mandela, Sumbawanga, mkoani Rukwa, umesogezwa mbele ili kuwapa fursa Biashara United kujiandaa kwa mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahaly Tripoli ya nchini Libya.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Benjami Mkapa jijini Dar es Salaam, Biashara waliibuka na ushindi wa 2-0.

Taarifa ya meneja wa Biashara United ya mkoani Mara, Frank Wambare aliyoitoa leo Jumatatu tarehe 18 Oktoba 2021, imeeleza wameipokea taarifa hiyo vizuri na kwa furaha na wataitumia vizuri nafasi hiyo kujiandaa vya kutosha iliwaweze kupata ushindi wa ugenini na kufuzu hatua inayofuata.

Pia, mda huo watatumia kushughulikia mambo ya usafiri kwani wanatarajia kuondoka nchini keshokutwa Jumatano au Alhamisi kwa ndege ya kuunga kwani hakuna ndege ya moja kwa moja. Aidha amesema, kambi inaendelea jijini Dar es Saalam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

error: Content is protected !!