Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kisa wafuasi wao kushikiliwa, Chadema watinga mahakamani
Habari za Siasa

Kisa wafuasi wao kushikiliwa, Chadema watinga mahakamani

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema
Spread the love

 

WANASHERIA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamewasilisha maombi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, kuiomba itoe amri ili wafuasi wake wanaoshikiliwa katika Kituo cha Polisi Mbweni, mkoani Dar es Salaam, wafikishwe mahakamani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu, leo Jumapili tarehe 3 Oktoba 2021, Afisa Habari wa Chadema Kanda ya Pwani, Gervas Lyenda, amesema maombi hayo yamewasilishwa kwa njia ya mtandao.

Lyenda amesema katika maombi hayo, wanaomba wanachama wao wanaoshikiliwa na polisi wapelekwe mahakamani kesho Jumatatu, tarehe 4 Oktoba 2021 au waachiwe bila masharti yoyote.

“Wanasheria wetu wa wakiongozwa na Alex Massaba, Dickson Matata na Michael Lugina, tayari wameshaomba Habeas Corpus (Amri ya Mahakama kutaka mahabusu wapelekwe mahakamani), ili wanachama wetu wanaoshikiliwa Mbweni wapelekwe mahakamani kesho Jumatatu au waachiwe bila masharti yoyote,” amesema Lyenda.

Lyenda amedai, wamechukua hatua hiyo baada ya juhudi za wanasheria wa Chadema kuwatafutia dhamana wanachama hao kugonga mwamba.

Jumla ya watu tisa wakiwemo wanachama na wafuasi wa Chadema Jimbo la Kawe, walikamatwa jana asubuhi walikamatwa na Jeshi la Polisi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam, wakiwa katika mazoezi (Jogging).

Miongoni mwao ni, Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Kibamba, Ernest Mgawe, aliyekamatwa baada ya kwenda kituoni hapo kumtolea dhamana mfanyakazi wake wa Mgawe Tv, mwanahabari Harlod Shemsanga.

Wengine ni, Katibu Mwenezi wa Chadema Kanda ya Pwani, Lilian Kimei na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Kichama wa Kinondoni, Rose Moshi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro, jana alinukuliwa na vyombo vya habari kwamba ni kweli wanachama hao wa Chadema walikamatwa.

Alisema walikamatwa baada ya kuona viashiria vyenye kupelekea uvunjifu wa amani kwa kutengeneza hisia zenye mitizamo ya kisiasa kupitia kivuli cha mazoezi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!