October 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mawaziri nane kuvamia vijijini 975

Spread the love

 

JUMLA ya Mawaziri nane wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanatarajia kuanza ziara ya siku 15 katika vijiji 975 kwa lengo la kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi. Anaripoti Mwandishi wetu (endelea…)

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi leo tarehe 3 Oktoba 2021, ziara hiyo inatarajiwa kuanza tarehe 5 hadi 20 Okotoba mwaka huu.

Taarifa hiyo iliyowekwa na wizara hiyo kwenye kwenye akaunti ya mtandao wa Twitter, imeainisha picha za mawaziri hao kuwa ni pamoja na waziri husika wa ardhi, William Lukuvi; Waziri wa afya maendeleo ya jamii wazee na watoto wa nchi hiyo, Ummy Mwalimu; Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda na Waziri wa Ulinzi, Dk. Stergomena Tax.

Wengine ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso; Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro; Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki.

Aidha, kufuatia ziara hiyo, baadhi ya wananchi wamewapongeza mawaziri hao kwa kuamuzi huo.

Mmoja wao ni Peter Sumbizi ambaye ameandika; Nawapongeza sana waheshimiwa mawaziri wa kisekta kwa kuanza ziara hiyo muhim! Migogoro ya ardhi ni mingi hapa nchini! Mungu awabariki mawaziri wote mtakapoanza ziara hiyo na zaidi sana Mheshimiwa Rais Samiah Suluhu Hassan

Wakati Mtenget Mghanga amesema “Kilimanjaro, Wilaya ya Mwanga mtafika lini ndugu waheshimiwa? Kuna mgogoro wa miaka mingi pale Mwanga mjini.”

error: Content is protected !!