Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia atoa mitihani mitano kwa NGO’s
Habari za Siasa

Rais Samia atoa mitihani mitano kwa NGO’s

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa mitihani mitano kwa mashirika yasiyo ya kiserikali nchini ikiwamo kuoanisha mipango yao na vipaumbele na mipango ya kitaifa. Anaripoti Helena Mkonyi, TUDARCo … (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 30 Septemba 2021 jijini Dodoma wakati akihutubia Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NaCONGO).

Ameagiza mashirika hayo kuusoma na kuutafsiri Mpango wa tatu wa Taifa wa miaka mitano katika kazi zao.

“Lengo ni kuutekeleza kwa pamoja serikali na ninyi ili tuende kufanya kazi ambayo tumekusudia kwa haraka katika mpango huo.

“Pili natoa wito kuongeza uwazi na uwajibika kwenye utendaji wa kazi zenu, mwanzo nimeeleza kuwa kuna mashirika yasiyo ya kiserikali zaidi ya 11000 yaliyosajiliwa lakini yanayofanya kazi ni 4663, hivyo kuna mashirika kama 7000 hayajulikani hayapo, yamekufa au vinginevyo.

“Hii ni kwa sababu mashirika mengi yanaanzishwa kwa ajenda iliyopo dunia kwa wakati ule, ulimwengu ukienda mazingira yatasajili mashirika ya mazingira. Ni kwa sababu wanajua fedha ipo pahali.

“Tuende kuendana na ajenda za ulimwengu mfano malengo endelevu na mpango wa serikali… tukienda hivyo wanaotoa fedha watakuelewa vizuri,” amesema

Tatu Rais Samia amehimiza mashirika ya ndani kupunguza utegemezi na kuagiza wizara ya afya kukaa na Baraza la mashirika hayo ili kutengeneza mpango mkakati ambao taasisi zitaweza kutafuta fedha zao na waweze kujitegemea.

“Nne, kama mnavyofahamu, nchi yetu ina utamaduni, mila na desturi zake hivyo basi natoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kufanya kazi zinazoendana na tamaduni, mila, desturi na maadili ya kitnzania. Vilevile nitoe wito kwa baraza kuendelea kuwahimiza wanachama wenu kuzingatia sheria inayosimamia shughuli za mashirika haya.

“Lakini pia naomba mhamasishe watu wajitokeze kwa wingi katika zoezi la sensa ya watu na makazi ambayo itafanyika mwaka kesho,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!