October 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yakamilisha muongozo wa misamaha ya kodi kwa NGO’s

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imeshakamilisha kitini kinachotoa muongozo wa namna mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s) yatanufaika na misamaha ya kodi. Anaripoti Glory Massamu, TUDARCo … (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 30 Septemba 2021 jijini Dodoma wakati akihutubia Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NaCONGO).

Amesema tayari Serikali iko katika hatua za za mwisho kumalizia muongozo huo.

Aidha, amesema changamoto ya ucheleweshwaji wa vibali vya kazi imetatuliwa kupitia mfumo wa kieletroniki ambao ulizinduliwa Aprili mwaka huu na Idara ya Uhamiaji hivyo kazi ni kwa muombaji kukamilisha taratibu zake.

“Pia nitoe rai kwa viongozi wa mamlaka ya serikali za mitaa kutoa ushirikiano wa kutosha mashirika haya na kufanya kazi kwa pamoja kwani kidole kimoja hakivunjia chawa,” amesema.

Aidha, ameagiza wizara ya afya kushirikiana na mashirika hayo katika mapambano dhidi ya Corona.

Awali Mwenyekiti Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NaCONGO), Dk. Lilian Badi mbali na kumpongeza Rais kwa juhudi za anazofanya kwenye janga la Corona, pia wapo tayari kuchangia uzoefu katika mapambano dhidi ya Corona.

Pia amesema wanachama wa baraza hilo wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali ikiwamo misamaha ya kodi kwa baadhi ya mashirika hayo na urasimu katika upatikanaji wa vibali kwa ajili ya kutekeleza miradi na afua mbalimbali.

error: Content is protected !!