Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wafuasi Chadema waangua kilio Mbowe akirudishwa rumande
Habari za SiasaTangulizi

Wafuasi Chadema waangua kilio Mbowe akirudishwa rumande

Spread the love

 

WAFUASI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wameangua kilio wakati mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, akirudishwa rumande katika gereza la Ukonga, anakoshikiliwa kutokana na mashtaka ya ugaidi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Tukio hilo limetokea leo Jumatatu, tarehe 30 Agosti 2021, baada ya Mbowe kutolewa katika kizimba cha Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam,  kwa ajili ya kupandishwa kwenye gari la Jeshi la Magereza, kurudishwa rumande.

Baada ya Mbowe kutoka nje ya geti la mahakama hiyo chini ya ulinzi mkali, wafuasi ambao walikuwa wanawake, walianza kulia wakisema mwanasiasa huyo sio gaidi, huku wengine wakimpa maneno ya faraja kwamba atashinda dhidi ya mashtaka yanayomkabili.

Mbowe alifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi aliyoifungua dhidi ya Serikali, akipinga utaratibu uliotumika kumfungulia kesi ya uhujumu uchumi, yenye mashtaka ya ugaidi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 23 Septemba 2021, ambapo mahakama hiyo itatoa uamuzi juu ya mapingazi manne, yaliyowekwa na upande wa Jamhuri, dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mbowe.

Mbowe na wenzake watatu, wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya kula njama za kufanya ugaidi, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa rasmi kesho Jumanne, tarehe 31 Agosti 2021, katika mahakama hiyo inayofahamika kwa jina la mahakama ya ufisadi.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni, Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Abdallah Ling’wenya.

Mkurugenzi wa Itifaki, mawasiliano na Mambo ya Nje Chadema, John Mrema amesema kesi hiyo itaanza kusikilizwa kesho ambapo Mbowe atafikishwa tena mahakamani hapo.

“Kesho siku ya kesi ya ugaidi itafanyika Mahakama Kuu maalum ya ufisadi, kesho ataletwa mahakamani saa tatu 3.00 asubuhi,” amesema Mrema.

Katika kesi hiyo, Mbowe na wenzake wanadaiwa kula njama za kufanya vitendo vya ugaidi, ikiwemo kulipua vituo vya mafuta na mikusanyiko ya watu, maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Kilimanjaro.

Pia, washtakiwa hao wanadaiwa kupanga njama za kutaka kuwadhuru viongozi wa Serikali, akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!