Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yaweka mapingamizi kesi ya Mbowe
Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaweka mapingamizi kesi ya Mbowe

Freeman Mbowe na wenzake wakiwa mahakamani Kisutu
Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imeweka mapingamizi manne katika kesi ya kikatiba, iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe akipinga utaratibu uliotumika kumkamata na kumfungulia mashtaka ya ugaidi katika mahakamani. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Katika kesi hiyo, Mbowe amemshtaki Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP), Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akidai walikiuka katiba, ikiwemo katika taratibu walizotumia kumkamata akiwa jijini Mwanza na kumfungulia mashtaka pasina kumpa hali ya kuwa na wakili wake wakati wa mahojiano.

Leo Jumatatu tarehe 30 Agosti 2021, wakati kesi hiyo iliposikilizwa mbele ya Jaji John Mgetta, Wakili wa  Serikali Mkuu, Hangi Chang’a, amesema Jamhuri imeamua kuweka mapingamizi manne, dhidi ya kesi hiyo.

Wakili Chang’a aliiomba mahakama hiyo isikilize mapingamizi hayo kwa njia ya maandishi.

Baada ya Wakili Chang’a kutoa ombi hilo, lililoafikiwa na upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Peter Kibatala, Jaji Mgeta alipanga tarehe 6 Septemba 2021, kuwa siku ya  upande wa Jamhuri kuwasilisha mapingamizi yao mahakamani hapo, kwa njia ya maandishi.

Pia, alipanga tarehe 9 Septemba 2021, kuwa siku ya upande wa utetezi kuwasilisha majibu yao dhidi ya mapingamizi hayo, kwa njia ya maandishi.

Jaji Mgetta aliipanga tarehe 23 Septemba 2021, kuwa siku ya mahakama hiyo kutoa uamuzi dhidi ya mapingamizi ya Jamhuri,  kuhusu kesi hiyo iliyofunguliwa na Mbowe.

Mbowe amefungua kesi hiyo  kupinga utaratibu uliotumiwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, kumkamata akiwa hotelini jijini humo, akijiandaa kushiriki kongamano la kudai katiba mpya lililoandaliwa na Chadema.

Pia, anapinga utaratibu uliotumika kumfungulia mashtaka ya ugaidi bila kumtaarifu kwa njia ya maandishi na kumwezesha kuwasiliana na wakili wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!