Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Upanuzi wa huduma kidijitali waendelea kunufaisha I& M Group PLC
Habari Mchanganyiko

Upanuzi wa huduma kidijitali waendelea kunufaisha I& M Group PLC

Mwenyekiti wa I&M Group PLC, Daniel Ndonye
Spread the love

 

KAMPUNI inayoongoza kwa utoaji wa huduma za fedha katika ukanda wa Afrika Mashariki, I&M Group PLC imetangaza kuongeza faida kwa asilimia 33 baada ya makato ya ushuru kwa mwaka wa fedha 2021 kutoka Sh. 67.5 bilioni hadi Sh. 88.6 bilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hadi kufikia juni mwaka jana, jumla ya mali za kampuni hiyo zimeweka rekodi kwa ukuaji wa asilimia 12 sawa na Sh trilioni nane kutoka Sh trilioni 7.1.

Hatua hiyo imekuja miezi michache baada ya kampuni hiyo kupanua huduma zake kwa upande wa nchi ya Uganda na kukaribisha wateja kukopa kwa wingi kutoka katika sekta binafsi na ya umma nchini humo.

Baada ya I&M Group PLC kutangaza kuichukua Benki ya Orient Limited (OBL) kwa asilimia kubwa huko nchini Uganda, kampuni hiyo iliongeza faida kwa Sh bilioni 496.

Akizungumzia kuhusu mtiririko wa fedha kutoka I&M Group PLC, Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Daniel Ndonye alisema malengo ya kampuni ni kuongezeka kwa utoaji wa mikopo kwa sekta binafsi na sekta ya umma.

Alisema utoaji huo wa mikopo ulionesha mwenendo wa benki hiyo kuendelea kukua licha ya kuwepo kwa changamoto za maambukizi ya virusi vya Corona.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Sarit Raja Shah alisisitiza uwekezaji mkubwa uliofanywa katika nusu ya kwanza ya 2021 kuendelea.

“Pamoja na ubunifu uliofanyika ndani ya soko pia tumeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika mifumo mipya ya kampuni kwa nia ya kuongeza ufanisi wa utendaji na kuboresha uzoefu wa benki juu ya wateja. ”

1 Comment

  • Mimi nimelazimika kuifunga akaunti yangu katika benki hii baada ya kugundua kuwa ina makato na tozo kibao. Ulimwenguni sijawahi kuona benki inayotoza kama hii pamoja na NMB. Hapa Tanzania kuna benki ambazo hazina makato na tozo kama I & M na NMB, Kwa hiyo wasijifanye wanatengeneza faida kubwa, Ni kwa sababu wanawakamua wateja wao

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!