Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Michezo Bayern yapiga 12 bila Lewandowsik
Michezo

Bayern yapiga 12 bila Lewandowsik

Spread the love

 

KLABU ya Bayern Munich imeibuka na ushindi wa mabao 12 -0 dhidi ya Bremer SV katika mchezo wa raundi ya kwanza ndani ya German Cup. Anaripoti Damas Ndelema, TUDACo … (endelea).

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Weserstadion, shujaa alikuwa ni Eric Maxim Choupo-Moting ambaye alitupia mabao manne dakika ya 8, 28, 35 na 82.

Mengine yalifungwa Jamal Musiala dakika 16 na 48, Jan -Luca Warm alijifunga dakika 27, Mali Tillman dakika 47, Leroy Sane dakika 65, Michael Cuisance dk 80, Bound Sarr dakika 86 na Corentin Tolisso dakika 88.

Katika mchezo huo Bayern Munich walitawala katika kila idara ambapo kwa upande wa mashuti yaliyoelekea langoni walipiga 37 huku wapinzani wao wakipiga mashuti 7 na katika mashuti hayo 37, 21 yalilenga lango na wapinzani wao Bremer SV ni shuti moja lililenga lango.

Umiliki wa mpira ilikuwa ni aslimia 68 kwa Bayern Munich na 32 kwa Bremer SV, pasi zilipigwa 612 upande wa Bayern Munich na 287 kwa Bremer SV.

Huo ni ushindi nwa kipekee kwa Bayerni bila ya kuwa na mshambuliaji wake hatari Robert Lewandowsik

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Jumamosi ya leo ni ya pesa tu kutoka Meridianbet

Spread the love  IKIWA leo hii ni Jumamosi nyingine na tulivu kabisa,...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

error: Content is protected !!